56. Kupangusa juu ya soksi za ngozi, soksi za kawaida na viatu

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

88 – Tunawapenda watu waadilifu na waaminifu, na tunawachukia watu wa dhuluma na khiyana.

89 – Katika yale ambayo hatuna uhakika nayo tunasema “Allaah ndiye mjuzi zaidi”.

90 – Tunaona kufaa kufuta juu ya soki za ngozi, ni mamoja wakati wa safari na mjini. Hivyo ndivyo imepokelewa.

MAELEZO

Kama waandishi wengine walioandika juu ya vitabu vya ´Aqiydah, mtunzi ameingiza suala la kufuta juu ya soksi za ngozi pasi na kutaja kufuta juu ya soksi za kawaida na viatu. Hilo ni kutokana na sababu mbili:

1 – Kupangusa juu ya soksi za ngozi ni jambo limepokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

2 – Raafidhwah wanapinga Sunnah hii. Kwa ajili hiyo hoja ni yenye nguvu zaidi dhidi yao kwa yale yaliyopokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu tu kumetajwa soksi za ngozi, haina maana kuwa kupangusa soksi za kawaida na viatu havikuthibiti. Unaweza kusoma kwa undani zaidi jambo hilo katika  ”al-Mas´h ´alaal-Jawrabayn” cha Shaykh al-Qaasimiy, ambacho nimekiambatanishia kiambatisho na hukumu kadhaa zinazohusiana na kupangusa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 81-82
  • Imechapishwa: 09/10/2024