Abul-Khattwaab [al-Kalwadhaaniy al-Hanbaliy] amesema:
“Imechukizwa kufanya vikao kwa ajili ya kutoa pole.”
Ibn ´Aqiyl amesema:
“Mikusanyiko imechukizwa baada ya roho kutoka. Kunasababisha tu huzuni zaidi.”
Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:
“Imechukizwa kuazi kwenye makaburi. Isipokuwa kwa yule ambaye hakutoa pole. Mtu kama huyu anaweza kuazi kabla ya mazishi au baada yake.”
Ahmad amesema:
“Ukitaka unaweza kumshika mkono yule aliyepatwa na msiba na ukampa pole na kama ukitaka usifanye hivo. Ukimwona yule aliyepatwa na msiba anararua nguo zake, mpe pole. Hatoacha haki kwa ajili ya batili. Ni vizuri ikiwa utamkataza.”
Ikiwa mkusanyiko una kumpa mawaidha na kumridhisha yule aliyepatwa na msiba na yote hayo yakamfanya kuliwazika katika kupitia zile Aayah na Hadiyth zinazozungumzia subira na kuridhia, ni sawa kukusanyika. Kutoa pole ni Sunnah iliyosuniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo mkusanyiko hautakiwi kuwa katika ile sura inayofanywa hii leo ambapo wanakaa kwa njia maalum na kusoma Qur-aan na ambayo mara nyingi hufanywa makaburini, nyumbani kwa wafiliwa au kwenye mikusanyiko mikubwa. Hii ni Bid´ah iliyochukiwa na Salaf lakini ambayo inawaliwaza wale waliofikwa na msiba na kuwafanya wakasahau huzuni na Allaah ndiye anajua zaidi.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 120-121
- Imechapishwa: 26/10/2016
Abul-Khattwaab [al-Kalwadhaaniy al-Hanbaliy] amesema:
“Imechukizwa kufanya vikao kwa ajili ya kutoa pole.”
Ibn ´Aqiyl amesema:
“Mikusanyiko imechukizwa baada ya roho kutoka. Kunasababisha tu huzuni zaidi.”
Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:
“Imechukizwa kuazi kwenye makaburi. Isipokuwa kwa yule ambaye hakutoa pole. Mtu kama huyu anaweza kuazi kabla ya mazishi au baada yake.”
Ahmad amesema:
“Ukitaka unaweza kumshika mkono yule aliyepatwa na msiba na ukampa pole na kama ukitaka usifanye hivo. Ukimwona yule aliyepatwa na msiba anararua nguo zake, mpe pole. Hatoacha haki kwa ajili ya batili. Ni vizuri ikiwa utamkataza.”
Ikiwa mkusanyiko una kumpa mawaidha na kumridhisha yule aliyepatwa na msiba na yote hayo yakamfanya kuliwazika katika kupitia zile Aayah na Hadiyth zinazozungumzia subira na kuridhia, ni sawa kukusanyika. Kutoa pole ni Sunnah iliyosuniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo mkusanyiko hautakiwi kuwa katika ile sura inayofanywa hii leo ambapo wanakaa kwa njia maalum na kusoma Qur-aan na ambayo mara nyingi hufanywa makaburini, nyumbani kwa wafiliwa au kwenye mikusanyiko mikubwa. Hii ni Bid´ah iliyochukiwa na Salaf lakini ambayo inawaliwaza wale waliofikwa na msiba na kuwafanya wakasahau huzuni na Allaah ndiye anajua zaidi.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 120-121
Imechapishwa: 26/10/2016
https://firqatunnajia.com/56-kukusanyika-kwa-ajili-ya-kutoa-pole/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)