211 – Ahmad bin al-Furaat ametukhabarisha: Aswbagh bin al-Faraaj ametukhabarisha: Ibn Wahb ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Ayyuub, kutoka kwa Abu Haaniy’, kutoka kwa kutoka kwa ´Amr bin Maalik, kutoka kwa Fadhwaalah bin ´Ubayd, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ee Allaah! Mwenye kukuamini na akashuhudia ya kwamba mimi ni Mtume Wako, basi ampendezee kukutana na Wewe, umfanyie wepesi hukumu Yako na umpunguzie maisha ya dunia. Na yule asiyekuamini na asishuhudie ya kwamba mimi ni Mtume Wako, basi usimpendezee kukutana na Wewe, usimfanyie wepesi hukumu Yako na muongezee maisha ya dunia.”[1]
212 – al-Huutwiy ametuhadithia: Baqiyyah ametukhabarisha, kutoka kwa Safwaan: Nimemsikia Shurahbiyl bin Ma´shar amesimulia kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna mja yeyote anapambana kutafuta kujionyesha na kusikika katika maisha ya dunia, isipokuwa Allaah atamfanya kusikika mbele ya viumbe siku ya Qiyaamah.”[2]
[1] Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” (208) na al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (1311).
[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4881).
- Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 56
- Imechapishwa: 20/07/2025
211 – Ahmad bin al-Furaat ametukhabarisha: Aswbagh bin al-Faraaj ametukhabarisha: Ibn Wahb ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Ayyuub, kutoka kwa Abu Haaniy’, kutoka kwa kutoka kwa ´Amr bin Maalik, kutoka kwa Fadhwaalah bin ´Ubayd, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ee Allaah! Mwenye kukuamini na akashuhudia ya kwamba mimi ni Mtume Wako, basi ampendezee kukutana na Wewe, umfanyie wepesi hukumu Yako na umpunguzie maisha ya dunia. Na yule asiyekuamini na asishuhudie ya kwamba mimi ni Mtume Wako, basi usimpendezee kukutana na Wewe, usimfanyie wepesi hukumu Yako na muongezee maisha ya dunia.”[1]
212 – al-Huutwiy ametuhadithia: Baqiyyah ametukhabarisha, kutoka kwa Safwaan: Nimemsikia Shurahbiyl bin Ma´shar amesimulia kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna mja yeyote anapambana kutafuta kujionyesha na kusikika katika maisha ya dunia, isipokuwa Allaah atamfanya kusikika mbele ya viumbe siku ya Qiyaamah.”[2]
[1] Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” (208) na al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (1311).
[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4881).
Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 56
Imechapishwa: 20/07/2025
https://firqatunnajia.com/55-duaa-kwa-ambaye-anamwamini-allaah-na-mtume-wake/