21 – Yule anayemtaja Allaah humpelekea kutajwa wakati wa shida. Imaam Ahmad amepokea ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Miongoni mwa yale mnayomtaja Allaah kwayo ikiwa ni pamoja na Tasbiyh, Tahmiyd na Tahliyl. Huzunguka karibu na ´Arshi zikiwa na sauti kama ya nyuki, zikimtaja yule aliyewatamka. Je, hapendi mmoja wenu awe na cha kumtaja nacho?”[1]
22 – Mja anapomjua Allaah katika hali ya raha kwa Dhikr, basi Allaah humjua katika hali ya dhiki. Kuna masimulizi yanayosema kwamba mja mtiifu na mwenye kumtaja Allaah akipata shida au akimuomba Allaah, Malaika husema:
“Ee Mola wetu! Sauti inayojulikana ya mja anayejulikana.”
Mja mwenye kughafilika akimuomba Allaah, Malaika husema:
“Ee Mola wetu! Sauti isiyojulikana ya mja asiyefahamika.”
23 – Inamwokoa mja na adhabu ya Allaah. Kama alivyosema Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna kitendo kilichofanywa na mwanadamu kinachomwokoa zaidi na adhabu ya Allaah kama kumtaja Allaah (Ta´ala).”
24 – Ni sababu ya kushuka kwa utulivu, kufunikwa na rehema na kuzungukwa na Malaika, kama alivyokhabarisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
25 – Ni sababu ya ulimi kushughulika mbali na usengenyi, umbea, uongo, matusi na batili. Kwani mja hawezi kuacha kuzungumza. Ikiwa hatamki Dhikr na amri za Allaah, basi atasema mambo ya haramu. Hakuna njia ya kuepuka hayo isipokuwa kwa Dhikr. Uzoefu na ushahidi vinasema hivyo. Mtu ambaye ulimi wake umezoea Dhikr, hulindwa na maneno ya batili. Na mwenye ulimi mkavu kutokamana na kumtaja Allaah, ulimi wake huteleza katika kila batili na maneno machafu.
26 – Vikao vya Dhikr ni vikao vya Malaika. Vikao vya batili na kughafilika ni vikao vya mashaytwaan. Hivyo basi mja achague ni kundi lipi la watu apende kuwa nao; atakuwa pamoja nao duniani na Aakhirah.
27 – Mtu anayemtaja Allaah hufurahia yeye mwenyewe na humfurahisha anayekaa naye. Huyu ndiye mwenye baraka popote alipo. Na mwenye kughafilika na kubwabwaja hujiletea huzuni yeye na anayeketi naye.
28 – Inamuepusha mja na majuto siku ya Qiyaamah. Kwani kila kikao ambacho mja hamtaji Allaah (Ta´ala) kitakuwa juu yake ni majuto siku hiyo.
29 – Ikiwa Dhikr hii imeandamana na kulia faraghani, basi humfanya mja kuwekwa chini ya kivuli cha ´Arshi ya Allaah (Ta´ala) siku ya jua kali na wakati watu wanachomwa na joto. Wakati watu wanayeyuka kwenye joto la jua katika kiwanja cha Mkusanyiko, basi mtu huyu anayefanya Dhikr atakingwa na kivuli cha ´Arshi ya Mwingi wa rehema (´Azza wa Jall).
[1] Ahmad (6/273), Ibn Maajah (3809) na al-Haakim (1/503), ambaye amesema kuwa ”Hadiyth iko kwa mujibu wa sharti za Muslim” na adh- Dhahabiy akaafikiana naye. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Mukhtaswar-ul-´Uluww” (32).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 97-99
- Imechapishwa: 18/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 97-99
Imechapishwa: 18/08/2025
https://firqatunnajia.com/54-sauti-isiyojulikana-kutoka-kwa-mtu-asiyejulikana/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket