54. Tofauti kati ya uombezi unaokubalika katika Shari´ah na wa shirki

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mlango wa tisa

Tofauti kati ya uombezi wa Kishari´ah na wa shirki

Akisema: “Je wewe unapinga uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuukana?” Mwambie: “Siupingi na wala siukani, bali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye muombezi wa waombezi na nataraji kupata uombezi wake.” Lakini uombezi wote [unamiliki] ni wa Allaah (Ta´ala). Kama alivyosema Allaah (Ta´ala):

قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا

“Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah pekee.”” (39:44)

MAELEZO

Bi maana mshirikina akikuuliza kama wewe unapinga uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anasema haya kwa sababu akulazimishe useme kuwa inafaa kumuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili akuombee mbele ya Allaah. Mwambie kuwa wewe hupingi na wala hukanushi uombezi wake. Pamoja na hivyo mwambie kuwa uombezi huu ni wa Allaah. Yeye ndiye Ambaye anautolea idhini pale Anapotaka na anampa Amtakaye. Allaah (Ta´ala) amesema:

قُل لِّلَّـهِ الشَّفَاعَةُ جَمِيعًا

“Sema: “Uombezi wote ni wa Allaah pekee.””

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 68
  • Imechapishwa: 24/11/2023