210 – al-Huutwiy ametukhabarisha: Baqiyyah ametukhabarisha: Buhayr ametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan, kutoka kwa Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa ´Awf bin Maalik, ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisimama mbele ya Maswahabah zake na akasema: ”Je, mnakhofia ufukara? Au yanakumsumbueni maisha ya dunia? Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) atakufungulieni ardhi ya Waajemi na Warumi.”[1]

[1] Ahmad (23462). Swahiyh kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (3257).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 55
  • Imechapishwa: 25/07/2025