1- Kuambiwa kutubia. Akitubia na akarudi katika Uislamu ndani ya siku tatu basi tawbah yake itakubaliwa kutoka kwake na ataachwa.

2-  Akikataa kutubia basi italazimika kumuua. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kubadilisha dini yake muueni.”[1]

3- Atazuiwa kuitumia mali yake ndani ya ule muda wa kumtubisha. Akitubia, basi hiyo ni mali yake, na akiendelea, basi itaingizwa katika wizara ya fedha ya waislamu na huku atauawa au atakufa akiwa ni mwenye kuritadi. Kuna maoni vilevile yanayosema kwamba kaunzia pale aliporitadi mali yake itaingizwa ndani ya manufaa ya waislamu.

4- Kutakatika kurithiana kati yake yeye na ndugu zake. Hiyo ina maana kwamba yeye hatowarithi na wao hawatomrithi.

5-  Akifa au akiuwawa kutokana na kuritadi kwake basi hatooshwa, hatoswaliwa na wala hatozikwa kwenye makaburi ya waislamu. Bali atazikwa katika makaburi ya makafiri au atachimbiwa shimo chini ya udongo sehemu yoyote kusipokuwa kwenye makaburi ya waislamu.

[1] Muslim (242).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 19/03/2020