Wengine wote wanaofungua wanawajibika kulipa siku walizofungua tu, isipokuwa yule aliyefungua kwa kufanya tendo la ndoa katika sehemu ya siri. Huyo atalipa siku hiyo na atamkomboa mtumwa. Ikiwa hatapata, basi atafunga miezi miwili mfululizo. Ikiwa hataweza, basi atawalisha masikini sitini. Ikiwa hatapata uwezo wa kufanya hivyo, basi wajibu huo huondoka kwake.
Ikiwa atafanya tendo la ndoa kisha asitoe kafara mpaka akafanya tendo la ndoa mara ya pili, anawajibika kafara moja tu. Ikiwa atatoa kafara kisha akafanya tendo la ndoa tena, anawajibika kafara nyingine. Kila anayewajibika kujizuia na kula na kunywa katika Ramadhaan kisha akafanya tendo la ndoa, basi anawajibika kutoa kafara.
Mwenye kuchelewesha kulipa siku za Ramadhaan kwa udhuru mpaka Ramadhaan nyingine ikamfikia, basi hana wajibu mwingine isipokuwa kulipa siku hizo. Lakini ikiwa alizembea bila udhuru, basi pamoja na kulipa siku hizo, atamlisha masikini mmoja kwa kila siku.
Ikiwa ataacha kulipa siku hizo mpaka akafa kwa sababu ya udhuru, basi hana chochote juu yake. Lakini ikiwa ilikuwa bila udhuru, basi kutatolewa chakula kumpa masikini mmoja kwa kila siku kwa niaba yake. Isipokuwa ikiwa funga hiyo ilikuwa ya nadhiri, katika hali hiyo hufungiwa kwa niaba yake. Hukumu ni hiyohiyo kwa kila nadhiri ya utiifu.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 41-42
- Imechapishwa: 02/11/2026
Wengine wote wanaofungua wanawajibika kulipa siku walizofungua tu, isipokuwa yule aliyefungua kwa kufanya tendo la ndoa katika sehemu ya siri. Huyo atalipa siku hiyo na atamkomboa mtumwa. Ikiwa hatapata, basi atafunga miezi miwili mfululizo. Ikiwa hataweza, basi atawalisha masikini sitini. Ikiwa hatapata uwezo wa kufanya hivyo, basi wajibu huo huondoka kwake.
Ikiwa atafanya tendo la ndoa kisha asitoe kafara mpaka akafanya tendo la ndoa mara ya pili, anawajibika kafara moja tu. Ikiwa atatoa kafara kisha akafanya tendo la ndoa tena, anawajibika kafara nyingine. Kila anayewajibika kujizuia na kula na kunywa katika Ramadhaan kisha akafanya tendo la ndoa, basi anawajibika kutoa kafara.
Mwenye kuchelewesha kulipa siku za Ramadhaan kwa udhuru mpaka Ramadhaan nyingine ikamfikia, basi hana wajibu mwingine isipokuwa kulipa siku hizo. Lakini ikiwa alizembea bila udhuru, basi pamoja na kulipa siku hizo, atamlisha masikini mmoja kwa kila siku.
Ikiwa ataacha kulipa siku hizo mpaka akafa kwa sababu ya udhuru, basi hana chochote juu yake. Lakini ikiwa ilikuwa bila udhuru, basi kutatolewa chakula kumpa masikini mmoja kwa kila siku kwa niaba yake. Isipokuwa ikiwa funga hiyo ilikuwa ya nadhiri, katika hali hiyo hufungiwa kwa niaba yake. Hukumu ni hiyohiyo kwa kila nadhiri ya utiifu.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 41-42
Imechapishwa: 02/11/2026
https://firqatunnajia.com/54-hukumu-zinazohusiana-na-kufungua-katika-ramadhaan/