Mwenye kula au kunywa, akatia dawa kupitia pua, akaingiza kitu chochote tumboni mwake kupitia sehemu yoyote, akajitapisha kwa makusudi, akajichua, akambusu au akamgusa mtu kisha akatokwa na manii, akatazama mara kwa mara mpaka akatoa manii au akapiga chuku kwa makusudi huku akikumbuka kuwa amefunga, basi swawm yake inaharibika. Ikiwa atafanya hayo kwa kusahau au kwa kulazimishwa, funga yake haiharibiki.
Ikiwa nzi ataingia kooni mwake, vumbi likafika kooni mwake, akasukutua au akavuta maji puani yakafika kooni mwake, akafikiri kisha akatoa manii, akaweka matone katika njia yake ya mkojo, akaota ndoto na akatokwa na manii au akashindwa kuzuia kutapika, basi funga yake haiharibiki.
Yule mwenye kula akidhani kuwa ni usiku kisha ikadhihirika kuwa ni mchana, basi ni wajibu kwake kulipa siku hiyo. Ikiwa atakula huku akiwa na shaka kama alfajiri imeingia, basi funga yake haiharibiki. Lakini ikiwa atakula huku akiwa na shaka kama jua limezama, basi ni wajibu kwake kulipa siku hiyo.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 42
- Imechapishwa: 02/11/2026
Mwenye kula au kunywa, akatia dawa kupitia pua, akaingiza kitu chochote tumboni mwake kupitia sehemu yoyote, akajitapisha kwa makusudi, akajichua, akambusu au akamgusa mtu kisha akatokwa na manii, akatazama mara kwa mara mpaka akatoa manii au akapiga chuku kwa makusudi huku akikumbuka kuwa amefunga, basi swawm yake inaharibika. Ikiwa atafanya hayo kwa kusahau au kwa kulazimishwa, funga yake haiharibiki.
Ikiwa nzi ataingia kooni mwake, vumbi likafika kooni mwake, akasukutua au akavuta maji puani yakafika kooni mwake, akafikiri kisha akatoa manii, akaweka matone katika njia yake ya mkojo, akaota ndoto na akatokwa na manii au akashindwa kuzuia kutapika, basi funga yake haiharibiki.
Yule mwenye kula akidhani kuwa ni usiku kisha ikadhihirika kuwa ni mchana, basi ni wajibu kwake kulipa siku hiyo. Ikiwa atakula huku akiwa na shaka kama alfajiri imeingia, basi funga yake haiharibiki. Lakini ikiwa atakula huku akiwa na shaka kama jua limezama, basi ni wajibu kwake kulipa siku hiyo.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 42
Imechapishwa: 02/11/2026
https://firqatunnajia.com/55-mambo-yanayoharibu-swawm/