53. Makundi ya watu wanaoruhusiwa kufungua Ramadhaan

Inaruhusiwa kufungua katika Ramadhaan kwa makundi manne:

1 – Mgonjwa ambaye kufunga kunamletea madhara na msafiri ambaye anaruhusiwa kufupisha swalah. Kwa hao wawili kufungua ni bora zaidi. Ni wajibu kwao kulipa siku walizofungua. Ikiwa watafunga, basi kufunga kwao kunatosheleza.

2 – Mwanamke mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi. Wao hufungua na hulipa siku hizo baadaye. Ikiwa watafunga, kufunga kwao hakutosihi.

3 – Mwanamke mjamzito na anayenyonyesha. Ikiwa watakhofia nafsi zao, basi watafungua na kulipa siku hizo baadaye. Ikiwa watawakhofia watoto wao, watafungua, watalipa siku hizo baadaye na watamlisha masikini mmoja kwa kila siku iliyowapita.

4 – Mtu asiyeweza kufunga kwa sababu ya uzee au ugonjwa ambao hautarajiwi kupona. Huyo atamlisha masikini mmoja kwa kila siku iliyowapita.

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 41
  • Imechapishwa: 02/11/2026