Ni wajibu kufunga Ramadhaan kwa kila muislamu aliyebaleghe, mwenye akili timamu na mwenye uwezo wa kufunga. Mtoto anaamrishwa kufunga anapokuwa na uwezo wa kufunga.
Kufunga Ramadhaan kunakuwa wajibu kwa mojawapo ya mambo matatu: kukamilika kwa mwezi wa Sha´baan, kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Ramadhaan au kuwepo kwa mawingu au vumbi jioni ya siku ya thelathini ambayo yanazuia kuuona mwezi.
Ikiwa mtu atauona mwezi mwandamo peke yake, basi atafunga. Ikiwa ni mtu mwadilifu, watu watafunga kwa ushahidi wake. Hawafungui mpaka washuhudiwe na watu wawili waadilifu. Mtu ambaye ameuuona mwezi mwandamo peke yake hafungui.
Ikiwa watafunga siku thelathini kwa ushahidi wa watu wawili, watafungua. Ikiwa wataanza kufunga kwa sababu ya mawingu au kwa maneno ya mtu mmoja, basi hawatafungua mpaka wauone mwezi mwandamo au watimize idadi ya siku.
Ikiwa miezi itamchanganyikia mfungwa aliye jela, atafanya jitihada ya kutafuta kujua mwezi uliopo kisha afunge. Ikiwa kufunga kwake kutalingana na mwezi wa Ramadhaan au mwezi uliofuata, kutamtosheleza. Ikiwa kutalingana na mwezi uliotangulia, hakutamtosheleza
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 41
- Imechapishwa: 01/11/2026
Ni wajibu kufunga Ramadhaan kwa kila muislamu aliyebaleghe, mwenye akili timamu na mwenye uwezo wa kufunga. Mtoto anaamrishwa kufunga anapokuwa na uwezo wa kufunga.
Kufunga Ramadhaan kunakuwa wajibu kwa mojawapo ya mambo matatu: kukamilika kwa mwezi wa Sha´baan, kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Ramadhaan au kuwepo kwa mawingu au vumbi jioni ya siku ya thelathini ambayo yanazuia kuuona mwezi.
Ikiwa mtu atauona mwezi mwandamo peke yake, basi atafunga. Ikiwa ni mtu mwadilifu, watu watafunga kwa ushahidi wake. Hawafungui mpaka washuhudiwe na watu wawili waadilifu. Mtu ambaye ameuuona mwezi mwandamo peke yake hafungui.
Ikiwa watafunga siku thelathini kwa ushahidi wa watu wawili, watafungua. Ikiwa wataanza kufunga kwa sababu ya mawingu au kwa maneno ya mtu mmoja, basi hawatafungua mpaka wauone mwezi mwandamo au watimize idadi ya siku.
Ikiwa miezi itamchanganyikia mfungwa aliye jela, atafanya jitihada ya kutafuta kujua mwezi uliopo kisha afunge. Ikiwa kufunga kwake kutalingana na mwezi wa Ramadhaan au mwezi uliofuata, kutamtosheleza. Ikiwa kutalingana na mwezi uliotangulia, hakutamtosheleza
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 41
Imechapishwa: 01/11/2026
https://firqatunnajia.com/52-hukumu-ya-kufunga-ramadhaan/