Zakaah haijuzu kupewa tajiri na wala kwa mwenye nguvu anayeweza kufanya kazi na kujipatia kipato. Wala haijuzu kwa watu wa familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nao ni Banuu Haashim na watu wao walioachwa huru. Wala haijuzu kupewa wazazi, hata kama ni wa juu zaidi, wala mtoto, hata kama ni wa chini zaidi, wala mtu ambaye unawajibika kumpa matumizi, wala kafiri. Ama swadaqah ya kujitolea, inajuzu kuwapa hawa na wengineo.
Haijuzu kutoa zakaah isipokuwa kwa nia, isipokuwa ikiwa mtawala ataichukua kwa nguvu.
Ikiwa atatoa zakaah kwa mtu ambaye hastahiki, basi haisihi. Isipokuwa ikiwa ni tajiri ambaye alimdhania kuwa ni fakiri.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 39-40
- Imechapishwa: 01/11/2026
Zakaah haijuzu kupewa tajiri na wala kwa mwenye nguvu anayeweza kufanya kazi na kujipatia kipato. Wala haijuzu kwa watu wa familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), nao ni Banuu Haashim na watu wao walioachwa huru. Wala haijuzu kupewa wazazi, hata kama ni wa juu zaidi, wala mtoto, hata kama ni wa chini zaidi, wala mtu ambaye unawajibika kumpa matumizi, wala kafiri. Ama swadaqah ya kujitolea, inajuzu kuwapa hawa na wengineo.
Haijuzu kutoa zakaah isipokuwa kwa nia, isipokuwa ikiwa mtawala ataichukua kwa nguvu.
Ikiwa atatoa zakaah kwa mtu ambaye hastahiki, basi haisihi. Isipokuwa ikiwa ni tajiri ambaye alimdhania kuwa ni fakiri.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 39-40
Imechapishwa: 01/11/2026
https://firqatunnajia.com/51-watu-ambao-haifai-kuwapa-zakaah/