Inajuzu kumpa mmoja wao zakaah yote. Dalili ya hilo ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamuru Banuu Zurayq watoe zakaah yao kumpa Salamah bin Sakhr[1]. Isitoshe alimwambia Qabiyswah:
“Subiri, ee Qabiyswah, mpaka zakaah itufikie, kisha tutakuamuru upewe.”[2]
Fakiri na masikini hupewa kile kiasi kinachokamilisha mahitaji yao. Mfanyakazi wa zakaah hupewa kiasi cha malipo ya kazi yake. Wale ambao nyoyo zao zinapendekezwa hupewa kiasi kitakachotimiza lengo la kuwapendezesha. Mtumwa anayefanya mkataba wa kujikomboa na mwenye deni hupewa kiasi kitakacholipa deni lake. Mpiganaji katika Njia ya Allaah hupewa kile anachohitaji kwa ajili ya vita yake. Msafiri aliyeishiwa na uwezo wa kuendelea na safari hupewa kiasi kitakachomfikisha katika mji wake. Hakuna hata mmoja wao anayezidishiwa zaidi ya kiasi hicho. Watu watano miongoni mwao hawapewi isipokuwa wanapokuwa na haja: fakiri, masikini, mtumwa anayefanya mkataba wa kujikomboa, mwenye deni kwa ajili yake mwenyewe na msafiri aliyeishiwa na uwezo wa kuendelea na safari. Watu wanne inajuzu kuwapa hata wakiwa matajiri: mfanyakazi wa zakaah, wale ambao nyoyo zao zinapendekezwa, mpiganaji katika Njia ya Allaah na mwenye deni kwa ajili ya kupatanisha baina ya watu.
[1] Abu Daawuud (2213) na at-Tirmidhiy (3299), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3299).
[2] Muslim (1044).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 39
- Imechapishwa: 01/11/2026
Inajuzu kumpa mmoja wao zakaah yote. Dalili ya hilo ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamuru Banuu Zurayq watoe zakaah yao kumpa Salamah bin Sakhr[1]. Isitoshe alimwambia Qabiyswah:
“Subiri, ee Qabiyswah, mpaka zakaah itufikie, kisha tutakuamuru upewe.”[2]
Fakiri na masikini hupewa kile kiasi kinachokamilisha mahitaji yao. Mfanyakazi wa zakaah hupewa kiasi cha malipo ya kazi yake. Wale ambao nyoyo zao zinapendekezwa hupewa kiasi kitakachotimiza lengo la kuwapendezesha. Mtumwa anayefanya mkataba wa kujikomboa na mwenye deni hupewa kiasi kitakacholipa deni lake. Mpiganaji katika Njia ya Allaah hupewa kile anachohitaji kwa ajili ya vita yake. Msafiri aliyeishiwa na uwezo wa kuendelea na safari hupewa kiasi kitakachomfikisha katika mji wake. Hakuna hata mmoja wao anayezidishiwa zaidi ya kiasi hicho. Watu watano miongoni mwao hawapewi isipokuwa wanapokuwa na haja: fakiri, masikini, mtumwa anayefanya mkataba wa kujikomboa, mwenye deni kwa ajili yake mwenyewe na msafiri aliyeishiwa na uwezo wa kuendelea na safari. Watu wanne inajuzu kuwapa hata wakiwa matajiri: mfanyakazi wa zakaah, wale ambao nyoyo zao zinapendekezwa, mpiganaji katika Njia ya Allaah na mwenye deni kwa ajili ya kupatanisha baina ya watu.
[1] Abu Daawuud (2213) na at-Tirmidhiy (3299), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (3299).
[2] Muslim (1044).
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 39
Imechapishwa: 01/11/2026
https://firqatunnajia.com/50-kiasi-wanachopewa-zakaa-wale-wastahiki/