Nao ni makundi aina nane:
1 – Mafukara. Nao ni wale ambao hawapati kitu cha kutosha kukidhi mahitaji yao, kupitia kazi wala kwa njia nyingine.
2 – Masikini. Nao ni wale ambao wanapata kiasi kinachoweza kukidhi baadhi ya mahitaji yao, lakini hawapati kinachotosheleza mahitaji yao yote.
3 – Wanaoshughulikia zakaah. Nao ni wale wanaokusanya zakaah na wale wanaohitajika katika kazi hiyo.
4 – Wale ambao nyoyo zao zinapendekezwa. Nao ni viongozi wenye kuheshimiwa na kutiiwa katika makabila yao ambao kwa kupewa zakaah yao kunatarajiwa kuzuia shari yao, kuimarisha imani yao, kuwazuia kuwadhuru waislamu au kuwasaidia kukusanya zakaah kutoka kwa wale wanaokataa kuitoa.
5 – Katika kuwaweka huru watumwa. Nao ni wale watumwa wanaofanya mkataba wa kujikomboa na kuwakomboa watumwa.
6 – Wenye madeni. Nao ni wale walio na madeni kwa ajili ya kujirekebisha wenyewe katika jambo linaloruhusiwa au kwa ajili ya kupatanisha baina ya makundi mawili ya waislamu.
7 – Katika Njia ya Allaah. Nao ni wapiganaji ambao hawana mgao maalum kutoka katika hazina ya waislamu.
8 – Msafiri aliyeishiwa na uwezo wa kuendelea na safari, hata ikiwa ni mwenye uwezo wa kifedha katika mji wake.
Hawa ndio watu wanaostahiki zakaah. Haifai kupewa zakaah mtu mwingine asiye miongoni mwao.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38-39
- Imechapishwa: 01/11/2026
Nao ni makundi aina nane:
1 – Mafukara. Nao ni wale ambao hawapati kitu cha kutosha kukidhi mahitaji yao, kupitia kazi wala kwa njia nyingine.
2 – Masikini. Nao ni wale ambao wanapata kiasi kinachoweza kukidhi baadhi ya mahitaji yao, lakini hawapati kinachotosheleza mahitaji yao yote.
3 – Wanaoshughulikia zakaah. Nao ni wale wanaokusanya zakaah na wale wanaohitajika katika kazi hiyo.
4 – Wale ambao nyoyo zao zinapendekezwa. Nao ni viongozi wenye kuheshimiwa na kutiiwa katika makabila yao ambao kwa kupewa zakaah yao kunatarajiwa kuzuia shari yao, kuimarisha imani yao, kuwazuia kuwadhuru waislamu au kuwasaidia kukusanya zakaah kutoka kwa wale wanaokataa kuitoa.
5 – Katika kuwaweka huru watumwa. Nao ni wale watumwa wanaofanya mkataba wa kujikomboa na kuwakomboa watumwa.
6 – Wenye madeni. Nao ni wale walio na madeni kwa ajili ya kujirekebisha wenyewe katika jambo linaloruhusiwa au kwa ajili ya kupatanisha baina ya makundi mawili ya waislamu.
7 – Katika Njia ya Allaah. Nao ni wapiganaji ambao hawana mgao maalum kutoka katika hazina ya waislamu.
8 – Msafiri aliyeishiwa na uwezo wa kuendelea na safari, hata ikiwa ni mwenye uwezo wa kifedha katika mji wake.
Hawa ndio watu wanaostahiki zakaah. Haifai kupewa zakaah mtu mwingine asiye miongoni mwao.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38-39
Imechapishwa: 01/11/2026
https://firqatunnajia.com/49-aina-ya-wanaostahiki-kupewa-zakaah/