Haijuzu kuichelewesha zakaah baada ya wakati wake wa kuwajibika ikiwa anaweza kuitoa. Akichelewesha kuitoa kisha mali ikapotea, bado itakuwa ni wajibu kwake kuitoa. Ikiwa mali itapotea kabla ya kuwajibika kutoa zakaah, basi hatoitolea zakaah.
Inajuzu kuitanguliza zakaah ikiwa kile kiwango chake kimekamilika. Lakini haijuzu kuitoa kabla ya kukamilika kwa kile kiwango chake. Ikiwa ataitanguliza na kumpa mtu ambaye hastahiki, haitamtosheleza, hata kama wakati wa kuwajibika zakaah huyo mtu atakuwa miongoni mwa wanaostahiki.
Ikiwa atampa zakaah mtu anayestahiki kisha akafa, akawa na uwezo wa kujitosheleza au akaritadi, basi zakaah hiyo imemtosheleza. Ikiwa mali itapotea, basi hatamdai aliyeipokea.
Haifai kuhamisha zakaah kwenda katika mji ambao swalah inafupishwa, isipokuwa ikiwa hatapata mtu wa kuipokea katika mji wake.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38
- Imechapishwa: 01/11/2026
Haijuzu kuichelewesha zakaah baada ya wakati wake wa kuwajibika ikiwa anaweza kuitoa. Akichelewesha kuitoa kisha mali ikapotea, bado itakuwa ni wajibu kwake kuitoa. Ikiwa mali itapotea kabla ya kuwajibika kutoa zakaah, basi hatoitolea zakaah.
Inajuzu kuitanguliza zakaah ikiwa kile kiwango chake kimekamilika. Lakini haijuzu kuitoa kabla ya kukamilika kwa kile kiwango chake. Ikiwa ataitanguliza na kumpa mtu ambaye hastahiki, haitamtosheleza, hata kama wakati wa kuwajibika zakaah huyo mtu atakuwa miongoni mwa wanaostahiki.
Ikiwa atampa zakaah mtu anayestahiki kisha akafa, akawa na uwezo wa kujitosheleza au akaritadi, basi zakaah hiyo imemtosheleza. Ikiwa mali itapotea, basi hatamdai aliyeipokea.
Haifai kuhamisha zakaah kwenda katika mji ambao swalah inafupishwa, isipokuwa ikiwa hatapata mtu wa kuipokea katika mji wake.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38
Imechapishwa: 01/11/2026
https://firqatunnajia.com/48-wakati-wa-kutoa-zakaah/