Hiyo ni wajibu kwa kila muislamu ambaye anamiliki ziada ya chakula chake na chakula cha wale anaowalisha katika usiku wa ´Iyd na mchana wake.
Kiwango cha zakaah ya mfunguo wa Ramadhaan ni pishi moja ya ngano, shayiri, unga wa ngano, unga wa shayiri, unga uliokaangwa, tende au zabibu kavu. Ikiwa hatapata chochote kati ya hivyo, basi atatoa pishi moja ya chakula chake, chochote kile.
Ambaye anawajibika kujitolea mwenyewe zakaah ya Fitwr yake, basi inakuwa wajibu kwake pia kumtolea yule ambaye matumizi yake yanamlazimu kuyabeba katika usiku wa ´Iyd, ikiwa anamiliki kiasi cha kutoa kwa niaba yake. Ikiwa matumizi ya mtu yanawajibika kwa kundi la watu – kama vile mtumwa anayemilikiwa kwa pamoja au ndugu wa karibu asiye na uwezo wa kujigharamia anayelazimikiwa kugharamiwa na kundi la watu – basi zakaah ya Fitwr yake ni juu yao kulingana na sehemu ya matumizi yake. Ikiwa mtu ni huru kwa sehemu na ni mtumwa kwa sehemu, basi zakaah ya Fitwr yake ni juu yake na juu ya bwana wake.
Inapendekezwa kutoa zakaah ya Fitwr siku ya ´Iyd kabla ya swalah. Haijuzu kuichelewesha baada ya siku ya ´Iyd. Inajuzu kuitoa siku moja au siku mbili kabla ya ´Iyd. Inafaa kumpa mtu mmoja kile kiasi kinachowajibika kwa kundi la watu, na kundi la watu kuwapa mtu mmoja kile kiasi kinachomlazimu mtu huyo mmoja.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38
- Imechapishwa: 01/11/2026
Hiyo ni wajibu kwa kila muislamu ambaye anamiliki ziada ya chakula chake na chakula cha wale anaowalisha katika usiku wa ´Iyd na mchana wake.
Kiwango cha zakaah ya mfunguo wa Ramadhaan ni pishi moja ya ngano, shayiri, unga wa ngano, unga wa shayiri, unga uliokaangwa, tende au zabibu kavu. Ikiwa hatapata chochote kati ya hivyo, basi atatoa pishi moja ya chakula chake, chochote kile.
Ambaye anawajibika kujitolea mwenyewe zakaah ya Fitwr yake, basi inakuwa wajibu kwake pia kumtolea yule ambaye matumizi yake yanamlazimu kuyabeba katika usiku wa ´Iyd, ikiwa anamiliki kiasi cha kutoa kwa niaba yake. Ikiwa matumizi ya mtu yanawajibika kwa kundi la watu – kama vile mtumwa anayemilikiwa kwa pamoja au ndugu wa karibu asiye na uwezo wa kujigharamia anayelazimikiwa kugharamiwa na kundi la watu – basi zakaah ya Fitwr yake ni juu yao kulingana na sehemu ya matumizi yake. Ikiwa mtu ni huru kwa sehemu na ni mtumwa kwa sehemu, basi zakaah ya Fitwr yake ni juu yake na juu ya bwana wake.
Inapendekezwa kutoa zakaah ya Fitwr siku ya ´Iyd kabla ya swalah. Haijuzu kuichelewesha baada ya siku ya ´Iyd. Inajuzu kuitoa siku moja au siku mbili kabla ya ´Iyd. Inafaa kumpa mtu mmoja kile kiasi kinachowajibika kwa kundi la watu, na kundi la watu kuwapa mtu mmoja kile kiasi kinachomlazimu mtu huyo mmoja.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 38
Imechapishwa: 01/11/2026
https://firqatunnajia.com/48-zakaah-ya-fitwr/