54. Du´aa wakati wa kuhisi maumivu maeneo fulani mwilini II

138 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaaa) amesimulia: “Wakati mtu anapomlalamikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya jambo fulani, kidonda au akawa na jeraha, basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hufanya kwa kidole chake namna hii – Sufyaan akaweka kidole chake cha shahaadah ardhini – kisha akakinyanyua na kusema:

بِاسْمِ اللَّهِ، تُرْبَةُ أَرْضِنَا بِرِيقَةِ بَعْضِنَا ، لِيُشْفَى بِهِ سَقِيمُنَا بِإِذْنِ رَبِّنَا

“Kwa jina la Allaah, mchanga ya ardhi yetu na kwa mate ya baadhi yetu, yanaponyesha mgonjwa wetu, kwa idhini ya Mola wetu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna uwekwaji Shari´ah wa kitendo hichi, nacho ni kuchukua mate kidogo kwa kidole chake cha shahaadah kisha akakiweka kwenye mchanga. Inahusiana na mchanga wowote ikiwa ni msafi. Baada ya hapo atakiweka mahali anapohisi maumivu hali ya kuwa ni mwenye kusema wakati wa kupangusa:

بِاسْمِ اللَّهِ، تُرْبَةُ أَرْضِنَا بِرِيقَةِ بَعْضِنَا ، لِيُشْفَى بِهِ سَقِيمُنَا بِإِذْنِ رَبِّنَا

“Kwa jina la Allaah, mchanga ya ardhi yetu na kwa mate ya baadhi yetu, yanaponyesha mgonjwa wetu, kwa idhini ya Mola wetu.”

Kama ilivyopokelewa katika Hadiyth.

[1] al-Bukhaariy (5745) na Muslim (2194).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 133
  • Imechapishwa: 12/11/2025