al-´Ayyaashiy amesema alipokuwa akifasiri Aayah:
شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ
“Allaah ameshuhudia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye na Malaika na wenye elimu [pia wamefanya hali kadhalika], ni Mwenye kusimamisha kwa uadilifu.”[1]
Amesema[2]:
وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ
“… na wenye elimu [pia wamefanya hali kadhalika], ni Mwenye kusimamisha kwa uadilifu.”
“Wenye elimu ni Mitume na wale waliopewa wasia. Wamesimamisha kwa uadilifu. [Maana yake ya] udhahiri ni uadilifu na ya undani ni kiongozi wa waumini.”
Marzabaan al-Qummiy amesema: “Nilimuuliza Abul-Hasan kuhusiana na Aayah:

“Allaah ameshuhudia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye na Malaika na wenye elimu [pia wamefanya hali kadhalika], ni Mwenye kusimamisha kwa uadilifu.”[3]
Akasema: “Ni imamu.”[4]
Kusimamisha kwa uadilifu katika Aayah ni sifa ya Allaah. Yeye (Subhaanah) ndiye Mwenye kusimamisha kwa uadilifu katika mambo yote.
Tafsiri ya mtu huyu ni tafsiri ya batili na imejengwa juu ya matamanio. Tafsiri yake:
“[Maana yake ya] udhahiri ni uadilifu na ya undani ni kiongozi wa waumini.”
ni tafsiri ya ki-Baatwiniyyah na kikafiri. Huku ni kufanya mzaha na kucheza na Qur-aan na wanacheza na akili za Raafidhwah. Allaah amemtakasa Abu Ja´far na waumini wengine wote kutokamana na hayo. Maneno Yake:
“Wenye elimu ni Mitume na wale waliopewa wasia.”
ni batili. Allaah ameteremsha Qur-aan ili watu wote waweze kuongozwa nayo. Ameamrisha irejelewe, ifuatwe na ishikwe. Elimu na uongofu wake haukuishilia kwa wausiwa wa uongo. Katika Ummah huu kuna mabinjwa na wanachuoni tele kabisa na katika msitari wa mbele kabisa ni Maswahabah watukufu na Taabi´uun wema na wenye kuwafuata kwa wema mpaka hii leo.
Kilicho cha ajabu ni namna Raafidhwah wanavyowapambanua wausiwa kwa elimu kisha wanadai kuwa wameficha Qur-aan na elimu walionayo. Ni ipi basi faida ya kufanya elimu imekomeka kwao? Iko wapi faida kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumwa kwa walimwengu wote kufikisha bishara njema na kuonya? Ina maana kwamba kazi ya wausiwa ni kuubomoa Uislamu.
[1] 03:17
[2] Bi maana Abu Ja´far.
[3] 03:17
[4] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/166).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 86-87
- Imechapishwa: 03/04/2017

Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 86-87
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/54-al-ayyaashiy-upotoshaji-wake-wa-pili-wa-aal-imraan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)