53. Du´aa wakati wa kuhisi maumivu maeneo fulani mwilini

137 – ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw ath-Thaqafiy amesimulia: “Nilimshtakia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maumivu ninayohisi mwilini mwangu tangu niliposilimu.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Weka mkono wako pale mahali unapohisi maumivu katika mwili wako, useme mara tatu:

باسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

kisha useme mara saba:

أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ

“Najilinda kwa Allaah na kwa uwezo Wake kutokamana na shari ya ninachokihisi na ninachokitahadhari.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna uwekwaji Shari´ah wa mtu kuweka mkono wake pale mahali anapohisi maumivu mwilini mwake na aseme Dhikr hii mara tatu:

باسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

kisha useme mara saba:

أَعُوذُ بِاللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ

“Najilinda kwa Allaah na kwa uwezo Wake kutokamana na shari ya ninachokihisi na ninachokitahadhari nacho.”

Imekuja katika tamko jengine:

أَعُوذُ بِعِزَّةِ اللَّهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأَحَاذِرُ

“Najilinda kwa utukufu wa Allaah na kwa uwezo Wake kutokamana na shari ya ninachokihisi na ninachokitahadhari nacho.”[2]

[1] Muslim (2203).

[2] Abu Daawuud (3891), at-Tirmidhiy (2080) na Ibn Maajah (3522).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 132
  • Imechapishwa: 12/11/2025