Kuna Hadiyth nyingi zinathibitisha mkono wa Allaah. Hapa kunafuatia baadhi ya maneno ya maimamu kuhusu mtu anatakiwa achukue msimamo gani juu ya sifa za Allaah (´Azza wa Jall):
54- Baqiyyah ameeleza kwamba al-Awzaa´iy amesema:
“az-Zuhriy na Mak-huul walikuwa wakisema: “Zipitisheni Hadiyth hizi kama zilivyokuja.”
55- al-Waliyd bin Muslim amesimulia:
“Nilimuuliza Maalik bin Anas, Sufyaan ath-Thawriy, al-Layth bin Sa´d na al-Awzaa´iy kuhusu Hadiyth zinazoongelea sifa. Wakasema: “Zipitisheni kama zilivyokuja.”
56- al-Laalakaa´iy amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Muhammad bin al-Hasan ash-Shaybaaniy, mwanafunzi wa Abu Haniyfah, ambaye amesema:
“Wanachuoni wote Mashariki na Magharibi wameafikiana juu ya kuamini Qur-aan na Sunnah zilizopokelewa na wapokezi waaminifu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu sifa za Mola (´Azza wa Jall) pasi na tafsiri, kuzielezea wala kuzifananisha. Yule mwenye kufasiri kitu katika hayo basi ametoka na yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amefarikiana na mkusanyiko. Yule mwenye kusema yale yaliyosemwa na Jahm basi amefarikiana na mkusanyiko. Kwa sababu amemweleza kwa sifa isiyokuwa chochote.”
57- al-Awzaa´iy amesema:
“Lazimiana na mapokezi ya waliotangulia japokuwa utakataliwa na watu. Na tahadhari na maono ya watu japokuwa watakupambia kwa maneno.”
58- Imepokelewa kwamba al-Hasan al-Baswriy amesema:
“Mutwarrif amezungumza maneno ambayo hayajasemwa na yeyote kabla wala baada yake. Wakasema: “Amesema nini, ee Abu Sa´iyd?” Akasema: “Shukurani zote njema anastahiki ambaye miongoni mwa kumuamini ni kuwa mjinga juu ya yale aliyojisifu nafsi Yake.”
- Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 36-37
- Imechapishwa: 14/07/2019
Kuna Hadiyth nyingi zinathibitisha mkono wa Allaah. Hapa kunafuatia baadhi ya maneno ya maimamu kuhusu mtu anatakiwa achukue msimamo gani juu ya sifa za Allaah (´Azza wa Jall):
54- Baqiyyah ameeleza kwamba al-Awzaa´iy amesema:
“az-Zuhriy na Mak-huul walikuwa wakisema: “Zipitisheni Hadiyth hizi kama zilivyokuja.”
55- al-Waliyd bin Muslim amesimulia:
“Nilimuuliza Maalik bin Anas, Sufyaan ath-Thawriy, al-Layth bin Sa´d na al-Awzaa´iy kuhusu Hadiyth zinazoongelea sifa. Wakasema: “Zipitisheni kama zilivyokuja.”
56- al-Laalakaa´iy amepokea kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa Muhammad bin al-Hasan ash-Shaybaaniy, mwanafunzi wa Abu Haniyfah, ambaye amesema:
“Wanachuoni wote Mashariki na Magharibi wameafikiana juu ya kuamini Qur-aan na Sunnah zilizopokelewa na wapokezi waaminifu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu sifa za Mola (´Azza wa Jall) pasi na tafsiri, kuzielezea wala kuzifananisha. Yule mwenye kufasiri kitu katika hayo basi ametoka na yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amefarikiana na mkusanyiko. Yule mwenye kusema yale yaliyosemwa na Jahm basi amefarikiana na mkusanyiko. Kwa sababu amemweleza kwa sifa isiyokuwa chochote.”
57- al-Awzaa´iy amesema:
“Lazimiana na mapokezi ya waliotangulia japokuwa utakataliwa na watu. Na tahadhari na maono ya watu japokuwa watakupambia kwa maneno.”
58- Imepokelewa kwamba al-Hasan al-Baswriy amesema:
“Mutwarrif amezungumza maneno ambayo hayajasemwa na yeyote kabla wala baada yake. Wakasema: “Amesema nini, ee Abu Sa´iyd?” Akasema: “Shukurani zote njema anastahiki ambaye miongoni mwa kumuamini ni kuwa mjinga juu ya yale aliyojisifu nafsi Yake.”
Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 36-37
Imechapishwa: 14/07/2019
https://firqatunnajia.com/52-namna-hii-ndivo-walivyoamini-maimamu-mashariki-na-magharibi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)