52. Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni shirki

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hivyo mwambie: “Kwa hiyo ukitambua maneno ya Allaah (Ta´ala):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

“Basi swali na chinja kwa ajili ya Mola Wako.” (108:02)

ukamtii Allaah na ukamchinjia; je hii ni ´ibaadah?” Hana budi kusema: “Ndio”. Hivyo muulize:

“Ukichinja kwa ajili ya kiumbe; ni mamoja awe ni Mtume, jini au mwengine; je utakuwa umeshirikisha katika ´ibaadah hii asiyekuwa Allaah?” Hana budi kukubali na kusema: “Ndio”.

MAELEZO

Hapa mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) anaenda katika aina nyingine ya ´ibaadah, ambayo ni kuchinja. Mwambie: “Kwa hiyo ukitambua maneno ya Allaah (Ta´ala):

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ

“Basi swali na chinja kwa ajili ya Mola Wako.”

ukimtii Allaah na ukamchinjia; je hii ni ´ibaadah?” Hana budi kusema: “Ndio”. Amekubali mwenyewe kuwa kuchinja kwa ajili ya Allaah (Ta´ala) ni ´ibaadah. Kujengea juu ya hili, kuchinja kwa ajili ya mwingine asiyekuwa Allaah inakuwa shirki.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 67
  • Imechapishwa: 24/11/2023