52. Maneno yanayopandishwa kwenda katika uso wa Allaah

49 – Abu Ahmad al-´Assaal amepokea kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwa Ibn Mas´uud ya kwamba amesema:

”Mwenye kusema:

سبحان الله و الحمد لله و الله اكبر

”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu. Himdi zote njema anastahiki Allaah. Allaah ni mkubwa.”,

basi anayapokea Malaika na kupanda nayo kwa Allaah (´Azza wa Jall). Hawapitii kundi lolote la Malaika isipokuwa wanamuombea msamaha aliyeyatamka mpaka pale anapofika nayo kwenye uso wa Mwingi wa huruma (´Azza wa Jall).”

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 104
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy