52. Kitenguzi cha tatu: Yule asiyewakufurisha makafiri basi naye ni kafiri

Shaykh na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

La tatu:

Yule asiyewakufurisha washirikina [makafiri], akawa na shaka juu ya ukafiri wao au akaona kuwa madhehebu/dini yao ni sahihi, amekufuru.

MAELEZO

La tatu – Bi maana miongoni mwa vitenguzi vya Uislamu.

Yule asiyewakufurisha washirikina – Kwa sababu ni wajibu kwa muislamu amkufurishe yule ambaye Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamemkufurisha. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewakufurisha washirikina; waabudu masanamu na wengineo ambao wanaabudu wengine pamoja na Allaah, na amemkufurisha yule asiyewaamini Mitume au baadhi yao katika ilivyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Kawakufurisha washirikina katika mayahudi, manaswara na waabudu mizimu. Kwa hiyo ni wajibu kwa muislamu kuamini ndani ya moyo wake kuwa ni makafiri kwa kutendea kazi ukafirishaji wa Allaah kwao na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala):

لَّقَدْ كَفَرَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الْمَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ

”Hakika wamekufuru wale ambao wamesema: “Hakika Allaah ni al-Masiyh mwana wa Maryam.” (al-Maaidah 05:17)

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا

”Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” [Sivyo kabisa, bali] mikono yao ndio ilivyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema.” (al-Maaidah 05:64)

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ

”Hakika Allaah ameisikia kauli ya wale ambao wamesema: “Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.” (Aal ´Imraan 03:181)

Kuna Aayah zengine ambazo Allaah amezisimulia kuwahusu wao.  Hawa ni Ahl-ul-Kitaab. Inatosha kuwakufurisha kwa kule kumkufuru kwao Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye Allaah amemtumiliza kwa watu wote. Wanapata hilo katika Tawraat na Injiyl. Amesema (Ta´ala):

النَّبِيَّ الْأُمِّيَّ الَّذِي يَجِدُونَهُ مَكْتُوبًا عِندَهُمْ فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ يَأْمُرُهُم بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَاهُمْ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ الطَّيِّبَاتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيْهِمُ الْخَبَائِثَ وَيَضَعُ عَنْهُمْ إِصْرَهُمْ وَالْأَغْلَالَ الَّتِي كَانَتْ عَلَيْهِمْ ۚ فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَقُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

“Mtume asiyejua kusoma wala kuandika ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl; anawaamrisha mema na maovu na anawahalalishia mazuri na anawaharamishia maovu na anawaondoshea mazito na minyororo iliyokuwa juu yao Hivyo basi, wale waliomwamini na wakamtukuza na wakamsaidia na wakafuata Nuru ambayo imeteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu. Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote Ambaye Pekee anao ufalme wa mbingu na ardhi.” (al-A´raaf 07:157-158)

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا

“Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote.”

ni yenye kuenea kwa watu wote wakiwemo watu wa Kitabu na wengineo:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنِّي رَسُولُ اللَّـهِ إِلَيْكُمْ جَمِيعًا الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرَسُولِهِ النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ الَّذِي يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَكَلِمَاتِهِ وَاتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

“Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote. Ambaye pekee yake Anao ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye; anahuisha na anafisha. Hivyo basi mwaminini Allaah na Mtume, asiyejua kusoma wala kuandika, ambaye anamwamini Allaah na maneno Yake na mfuateni ili mpate kuongoka.” (al-A´raaf 07:158)

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا

”Hatukukutuma isipokuwa kwa watu wote na uwe mbashiriaji na muonyaji.” (Sabaa´ 34:28)

Yule asiyeamini kwamba ujumbe wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa watu wote, hata kama atakubali ya kwamba ni Mtume wa Allaah lakini akaona kwamba jumbe wake ni kwa waarabu peke yao pasi na wengine, basi huyu ni kafiri. Vipi kwa yule ambaye anakufuru kabisa ujumbe wake na wala hautambui ujumbe wake. Huyu ni kafiri zaidi.

Kwa hiyo yule mwenye mashaka juu ya ukafiri wa washirikina kwa jumla, sawa ikiwa ni waabudu masanamu, mayahudi na manaswara au wale wanaojinasibisha na Uislamu wakati huohuo wanamshirikisha Allaah, ni wajibu kuamini kwamba ni makafiri. Kila yule ambaye anamshirikisha Allaah na akamuabudu pamoja Naye wengine katika miti, mawe, masanamu, makaburi na vyenginevyo, basi huyo ni mshirikina na ni kafiri. Ni wajibu kuonelea kuwa ni kafiri ijapokuwa atakuwa ni mwenye kudai Uislamu na anasema ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wake. Kwa sababu shirki inatilisha shahaadah mbili na inavunja Uislamu na inaiharibu Tawhiyd.

Kwa hivyo ni wajibu kwa muislamu kuwakufurisha washirikina ambao wanamuabudu asiyekuwa Allaah. Ni mamoja wakiwa ni waarabu au wasiokuwa waarabu. Ni mamoja wakiwa mayahudi au manaswara au wale wanaojinasibisha na Uislamu. Hii ni ´Aqiydah na hakuna mambo ya kupakana mafuta. Yule asiyewakufurisha washirikina basi anaritadi na anakuwa kafiri mfano wao. Kwa sababu amefanya imani na kufuru kuwa ni kitu kimoja. Hatofautishi baina ya hili na hili. Huyu ni kafiri.

Hali kadhalika yule mwenye shaka juu ya ukafiri wa washirikina na kusema: “Mimi sijui kama kweli ni makafiri au si makafiri”. Kwa msemo mwingine akawa na mashaka. Mtu huyu anakuwa kafiri. Kwa sababu ni mwenye shaka baina ya kufuru na imani na wala hakutofautisha baina ya hili na hili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 79-80
  • Imechapishwa: 16/09/2018