Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kuna mmoja katika wao alikiri mwenyewe:
Nimetembelea vyuo vyote
na nikatupia jicho alama zote hizo
Na sikuona chochote isipokuwa kudangana
hali ya kuweka mkono kwenye kidevu au kung´ata meno nikijutia
MAELEZO
Mmoja katika wakuu wao wanasema kuwa katika maisha yake yote hakujifunza chochote cha kutegemea. Hakika si vyenginevyo aliishilia katika istilahi kama vile dutu, isiyo ya kimwili, mwili na mengineyo katika mambo ya kudangana ambayo hayapelekei katika uhakika wowote. Amewatembelea wasomi wao wote na masomo yao yote akitafuta uhakika lakini pasi na kufanikiwa. Kila mmoja alikuwa na njia yake mwenyewe. Ima baadhi katika wao wawe wamekanganyikiwa na hawajui washike njia gani, wengine wajutie kwa sababu wamejua kuwa ni wapotofu na wamepotea. Jambo lao liliishilia namna hiyo. Kwa sababu hawakutegemea Qur-aan, Sunnah na mfumo wa Salaf ambao unamwongoza mtu katika njia sahihi. Allaah (Ta´ala) amesema:
الر كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ
“Alif Laam Raa. Kitabu Tumekiteremsha kwako ili uwatoe watu katika viza kuwaingiza katika nuru kwa idhini ya Mola wao, waelekee katika njia ya Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”[1]
Watu walikiacha Kitabu hiki ambacho kwacho Allaah anawatoa watu kutoka katika viza na kuwaingiza katika nuru; kutoka katika viza vya kufuru, shaka na ujinga na kumwingiza mtu katika nuru ya elimu, imani, yakini na utambuzi. Zingatia namna ambavyo amefanya viza kuwa vingi na akaifanya nuru kuwa moja. Kwa sababu haki ni moja tu na ujinga ni viza vingi. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ
“Hii ndio njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate vichochoro [vinginevyo]; vikakufarikisheni na njia Yake!”[2]
Batili ni yenye kuenea na ni yenye matawi mengi ilihali haki ni moja na haitofautiani. Haki kamwe haipindi. Njia ya Allaah ni moja na vijia ni vingi kwa sababu kila mmoja anadai kuwa yeye ndiye yuko katika haki.
[1] 14:01
[2] 6:153
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 88-89
- Imechapishwa: 12/08/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket