52. Hakusemwi “as-Salaam iwe juu ya Allaah”

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

1- Imesihi kupokelewa kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Tulikuwa tunapokuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah tunasema: “as-Salaam iwe juu ya Allaah kutoka kwa waja Wake. as-Salaam iwe juu ya fulani na fulani.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Msisemi “as-Salaam iwe juu ya Allaah”. Kwani Allaah Yeye ndiye as-Salaam.”[1]

MAELEZO

1- Imesihi kupokelewa kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Tulikuwa tunapokuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah tunasema: “as-Salaam iwe juu ya Allaah kutoka kwa waja Wake. as-Salaam iwe juu ya fulani na fulani.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Msisemi “as-Salaam iwe juu ya Allaah”. Kwani Allaah Yeye ndiye as-Salaam.”

as-Salaam inaweza kuwa na maana mbili:

1- Amesalimika kutokamana na kila aina ya upungufu na aibu. Yeye ana ukamilifu usiokuwa na kikomo kwa njia zote katika dhati Yake, majina Yake, sifa Zake na matendo Yake.

2- Anawapa amani waja Wake. Kwa hivyo haitakiwi kusema “as-Salaam iwe juu ya Allaah”. Kwani hii ni du´aa na Allaah ni mkwasi asiyehitajia kitu. Hana haja ya maombi ya watu. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kumuadhimisha na kumtakasa na kuamini kwamba ni Mwenye kusifiwa kwa sifa kamilifu na kwamba Yeye ni Mwenye kufanya vizuri na Mwenye kudhuru.

Hata hivyo ni sawa kusema “as-Salaam juu ya baadhi ya viumbe” kwa sababu ni wenye kuhitajia afya na du´aa.

Kusema kwamba lau kama si Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi tusingeongoka hakuna neno iwapo mtu anakusudia ulinganizi wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vinginevyo bora zaidi ni kusema “lau kama si Allaah kisha ulinganizi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi tusingeongoka”.

[1] al-Bukhaariy (835) na Muslim (402).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 152
  • Imechapishwa: 06/11/2018