Kuna zaidi ya faida mia za kumtaja Allaah ambapo baadhi yazo ni:
1 – Huufukuza, humwangusha na humvunja shaytwaan.
2 – Humridhisha Mwingi wa rehema (‘Azza wa Jall).
3 – Huondoa huzuni na dhiki kutoka moyoni.
4 – Huleta furaha, bashasha na upanuzi wa moyo.
5 – Huupa nguvu moyo na mwili.
6 – Huangaza uso na moyo.
7 – Huvutia riziki.
8 – Humvisha anayemtaja Allaah haiba, uzuri na mng’ao.
9 – Humletea mapenzi ya Allaah, ambayo ndiyo roho ya Uislamu, muhimili wa dini na njia ya furaha na wokovu. Hakika Allaah amekifanya kila kitu kuwa na sababu na akafanya sababu ya kupatikana mapenzi ya Allaah ni Dhikr ya kudumu. Hivyo basi ambaye anataka kupata mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na amtaje kwa wingi. Kwa hakika Dhikr ni kama kujifunza na kurudia masomo. Kama ilivyo kuwa ni mlango wa elimu, basi Dhikr ni mlango wa mapenzi. Njia yake ni pana na barabara yake imenyooka zaidi.
10 – Inamletea mja hali ya kujichunga mpaka inamfikisha katika daraja ya Ihsaan, hapo humuabudu Allaah kana kwamba anamwona. Hapana njia kwa mtu kupumbaa na Dhikr kufikia daraja ya Ihsaan. Ni kama ambavyo hawezi aliye kukaa kufika nyumbani.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 94-95
- Imechapishwa: 18/08/2025
Kuna zaidi ya faida mia za kumtaja Allaah ambapo baadhi yazo ni:
1 – Huufukuza, humwangusha na humvunja shaytwaan.
2 – Humridhisha Mwingi wa rehema (‘Azza wa Jall).
3 – Huondoa huzuni na dhiki kutoka moyoni.
4 – Huleta furaha, bashasha na upanuzi wa moyo.
5 – Huupa nguvu moyo na mwili.
6 – Huangaza uso na moyo.
7 – Huvutia riziki.
8 – Humvisha anayemtaja Allaah haiba, uzuri na mng’ao.
9 – Humletea mapenzi ya Allaah, ambayo ndiyo roho ya Uislamu, muhimili wa dini na njia ya furaha na wokovu. Hakika Allaah amekifanya kila kitu kuwa na sababu na akafanya sababu ya kupatikana mapenzi ya Allaah ni Dhikr ya kudumu. Hivyo basi ambaye anataka kupata mapenzi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na amtaje kwa wingi. Kwa hakika Dhikr ni kama kujifunza na kurudia masomo. Kama ilivyo kuwa ni mlango wa elimu, basi Dhikr ni mlango wa mapenzi. Njia yake ni pana na barabara yake imenyooka zaidi.
10 – Inamletea mja hali ya kujichunga mpaka inamfikisha katika daraja ya Ihsaan, hapo humuabudu Allaah kana kwamba anamwona. Hapana njia kwa mtu kupumbaa na Dhikr kufikia daraja ya Ihsaan. Ni kama ambavyo hawezi aliye kukaa kufika nyumbani.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 94-95
Imechapishwa: 18/08/2025
https://firqatunnajia.com/52-dhikr-inamridhisha-muumba-na-kumvunja-shaytwaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket