Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
29 – ´Aaishah na Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) wameeleza:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaamka asubuhi akiwa na janaba inayotokana na jimaa, kisha akaoga na kufunga.”[1]
Kuna maafikiano juu yake.
MAELEZO
Maneno yao (Radhiya Allaahu ´anhumaa) waliposema:
”… kutokana na janaba na si kuota.”
maana yake ni kwamba anaamka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) asubunhi akiwa na janaba kutokana na kujamii na si kwa sababu ya kuota, kwa kuwa jambo hilo halitokei kwake kwa sababu ni miongoni mwa michezo ya shaytwaan, jambo ambalo Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) wametakaswa kutokana nalo. Ni tofauti na wale waliosema kuwa kuna uwezekano wa ndoto kwa Mitume kwa kuchukua kutoka katika maneno yake:
”… kutokana na janaba na si kuota.”
Wamesema kuwa lau kama ndoto haiwezi kumtokea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi uvuaji huu usingelikuwa na maana yoyote, na jibu ni lile lililotangulia.
Hadiyth ni dalili ya kusihi kwa swawm ya mtu aliye na janaba hata kama hakuoga isipokuwa baada ya kuchomoza kwa alfajiri. Waziri Ibn Hubayrah na baada yake an-Nawawiy, wametaja maafikiano ya wanazuoni juu ya hilo[2]. Hakika tofauti ilitokea katika suala hili mwanzoni mwa ummah huu. Hilo ni kutokana na yale aliyopokea Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Pindi mwito wa swalah ya asubuhi utaponadiwa na mmoja wenu akiwa na janaba, basi asifunge siku yake.”[3]
Abu Hurayrah alikuwa akitoa fatwa kwa hilo. Baadhi ya wanafunzi wa Maswahabah pia walikuwa wakionelea hivo, kama alivyotaja at-Tirmidhiy[4].
Kisha tofauti hiyo iliondoka na maafikiano yakathibitika juu ya yale yaliyotangulia. Abu Hurayrah akajirejea katika fatwa hiyo, kama ilivyothibiti ndani ya ”as-Swahiyh” mbili. Kuhusu Hadiyth hiyo imefutwa kwa Hadiyth za Umm Salamah na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhumaa), jambo hilo limenakiliwa na al-Bayhaqiy kutoka kwa Ibn-ul-Mundhir na vivyo hivyo amesmea al-Khattwaabiy[5].
Imesemekana vilevile ya kwamba Hadiyth hiyo ina uzito mdogo kwa kuwa imepingwa na Hadiyth yenye usahihi zaidi na hivyo inapewa kipaumbele. Hayo ndio maoni ya Bukhaariy ambaye, baada ya kupokea Hadiyth ya ´Aaishah na Umm Salamah na akataja yaliyopokewa kutoka kwa Abu Hurayrah, akasema:
“Ya kwanza ina msimamo madhubuti zaidi… ”
Kwa maana ya kwamba cheni yake ya wapokezi ni yenye nguvu zaidi.
”… kwa sababu imepokelewa kutoka kwao kupitia njia nyingi sana. Kiasi cha kwamba Ibn ´Abdul-Barr akasema: “Hakika imesihi na imepokelewa kwa mapokezi mengi.”
Ama kuhusu yale yaliyopokewa kutoka kwa Abu Hurayrah, imepokewa kuwa hakuisikia moja kwa moja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), bali aliisikia kupitia kwa al-Fadhwl na Usaamah.
[1] al-Bukhaariy (1926) na Muslim (1109).
[2] al-Ifswaah (01/244) na “Sharh Swahiyh Muslim” (07/231).
[3] al-Bukhaariy (04/143 – “Fath”), Ahmad ameipokea kwa cheni yenye kuungana (13/490) na Ibn Hibbaan (3485) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.
[4] Jaamiy’-ut-Tirmidhiy (03/149).
[5] as-Sunan al-Kubraa (04/215) na “Ma’aalim-us-Sunan” (03/266).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/69-71)
- Imechapishwa: 17/03/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/69-71)
Imechapishwa: 17/03/2025
https://firqatunnajia.com/51-hadiyth-mtume-wa-allaah-alikuwa-anaamka-asubuhi-akiwa-na-janaba/