Hadiyth ni dalili ya kufaa kuchelewesha kuoga josho la janaba na kwamba si lazima kufanya hivyo mara moja, jambo ambalo limeshatangulia katika mlango wa twahara.
Mwanamke mwenye hedhi analinganishwa na mtu aliye na janaba ikiwa damu yake imekatika na akaona usafi kabla ya alfajiri. Katika hali hiyo anapaswa kufunga pamoja na watu hata kama hakuoga isipokuwa baada ya kuchomoza kwa alfajiri, kwa sababu wakati huo yeye ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kufunga. Aidha anapaswa kuharakisha kuoga ili aswali Fajr katika wakati wake. Wanawake wenye damu ya uzazi wana hukumu moja sawa na wenye hedhi katika hilo.
Ikiwa mtu anayefunga ataota ndoto mchana wa Ramadhaan, basi ataoga na swawm yake itakuwa sahihi, kwa sababu hana utashi wala matakwa katika jambo hilo. Amesema (´Azza wa Jall):
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا
“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]
Na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] 02:286
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/71)
- Imechapishwa: 17/03/2025
Hadiyth ni dalili ya kufaa kuchelewesha kuoga josho la janaba na kwamba si lazima kufanya hivyo mara moja, jambo ambalo limeshatangulia katika mlango wa twahara.
Mwanamke mwenye hedhi analinganishwa na mtu aliye na janaba ikiwa damu yake imekatika na akaona usafi kabla ya alfajiri. Katika hali hiyo anapaswa kufunga pamoja na watu hata kama hakuoga isipokuwa baada ya kuchomoza kwa alfajiri, kwa sababu wakati huo yeye ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kufunga. Aidha anapaswa kuharakisha kuoga ili aswali Fajr katika wakati wake. Wanawake wenye damu ya uzazi wana hukumu moja sawa na wenye hedhi katika hilo.
Ikiwa mtu anayefunga ataota ndoto mchana wa Ramadhaan, basi ataoga na swawm yake itakuwa sahihi, kwa sababu hana utashi wala matakwa katika jambo hilo. Amesema (´Azza wa Jall):
لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا
“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[1]
Na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] 02:286
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/71)
Imechapishwa: 17/03/2025
https://firqatunnajia.com/52-mfungaji-kuchelewesha-kuoga-josho-la-janaba-kujisafisha-na-hedhi-na-nifasi-baada-ya-alfajiri/