51. Du´aa wakati wa kumtembelea mgonjwa

135 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwa bwana mmoja akimzuru:

لا بأْسَ طَهـورٌ إِنْ شـاءَ الله

“Hapana neno; [ugonjwa] ni kusafishwa [madhambi] – Allaah akitaka.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Ndani yake kuna uwekwaji Shari´ah wa kumuombea du´aa mgonjwa kwa kusema:

لا بأْسَ طَهـورٌ إِنْ شـاءَ الله

“Hapana neno; [ugonjwa] ni kusafishwa [madhambi] – Allaah akitaka.”

Hapana vibaya akizidisha du´aa nyenginezo zisizokuwa na ubaya wowote. Kwa mfano anaweza kusema:

شفاك الله

“Allaah akuponye.”

نسأل الله أن يشفيك ويعافيك

“Tunamuomba Allaah akusalimishe na akuponye.”

جمع الله لك بين الأجر والعافية

“Allaah akukusanyie kati ya ujira na usalama.”

[1] al-Bukhaariy (5662).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 130
  • Imechapishwa: 11/11/2025