50. Siku nzito kwa makafiri na nyepesi kwa waumini


Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametaja baragumu tatu:

1- Baragumu ya mfazaiko katika Suurah “an-Naml”:

وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ ۚ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ

“Siku itakayopulizwa baragumu, tahamaki watafazaika waliomo mbinguni na waliomo ardhini isipokuwa atakaye Allaah; na wote watamfikia hali ya kuwa duni wamedhalilika.”[1]

2- Baragumu ya kifo katika Suurah “az-Zumar”:

وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَصَعِقَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ إِلَّا مَن شَاءَ اللَّـهُ

“Itapulizwa katika baragumu, basi watazimia wale walioko mbinguni na ardhini isipokua amtakaye Allaah.”[2]

3- Baragumu ya kufufuliwa katika Suurah “az-Zumar”:

ثُمَّ نُفِخَ فِيهِ أُخْرَىٰ فَإِذَا هُمْ قِيَامٌ يَنظُرُونَ

“Kisha litapulizwa humo jengine, tahamaki hao wanasimama wakitazama.”[3]

Maneno yake:

“Jua litasogezwa karibu nao.”

Mpaka litakuwa katika kiwango cha maili moja. Lakini waumini watakuwa katika kivuli:

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ

“Hakika wenye kumcha Allaah wamo katika vivuli na chemchemu.”[4]

Hawatalihisi:

لَا يَحْزُنُهُمُ الْفَزَعُ الْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ

“Haitowahuzunisha mfazaiko mkubwa kabisa na Malaika watawapokea.”[5]

Waumini watakuwa ndani ya raha katika siku hiyo:

وَكَانَ يَوْمًا عَلَى الْكَافِرِينَ عَسِيرًا

“Itakuwa ni siku ngumu kwa makafiri.”[6]

Ni siku nzito kwa makafiri:

فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ

“Itakapopulizwa katika baragumu kwa sauti kali.”[7]

B maana baragumu.

فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ

”Basi hiyo itakuwa ni siku ngumu. Kwa makafiri si nyepesi.”[8]

Ama waumini itakuwa ni siku nyepesi kwao na watakuwa katika vivuli vya baridi.

Uwanja huu ni kwamba watakusanywa kwenye ardhi moja watamfuata yule mwenye kuwaita na watakuwa ni wenye kukodoa macho. Ni uwanja tambarare usiyokuwa na milima wala mabonde:

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْجِبَالِ فَقُلْ يَنسِفُهَا رَبِّي نَسْفًا فَيَذَرُهَا قَاعًا صَفْصَفًا لَّا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجًا وَلَا أَمْتًا يَوْمَئِذٍ يَتَّبِعُونَ الدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُ ۖ وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ لِلرَّحْمَـٰنِ فَلَا تَسْمَعُ إِلَّا هَمْسًا

“Wanakuuliza juu ya milima. Sema: “Mola wangu atayapeperusha vumbivumvi, kisha ataiacha ardhi kuwa tambarare, uwanda. Hutoona humo mdidimio wala mwinuko. Siku hiyo watamfuata mwitaji hakuna kumkengeuka; na sauti zote zitamnyenyekea Mwingi wa rehema, basi hutosikia isipokuwa mchakato wa nyayo.”[9]

Watasimama katika uwanja huu tambarare usiyokuwa na milima wala mabonde.

[1] 27:87

[2] 39:68

[3] 39:68

[4] 77:41

[5] 21:103

[6] 25:26

[7] 74:08

[8] 74:09-10

[9] 20:105-108

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 07/04/2021