50. Mahakimu wa duniani na Hakimu wa mbinguni

47 – ´Abdur-Rahmaan bin Ghunm amesimulia kuwa amemsikia ´Umar bin al-Khattwaaab akisema:

”Ole wa mahakimu wa ardhini ile Siku watayokutana na Hakimu wa mbinguni, isipokuwa yule aliyeamrisha uadilifu, akahukumu kwa haki, na si kwa matamanio, ujamaa, matakwa na khofu, na daima akakiweka Kitabu cha Allaah mbele ya macho yake.”

Ibn Ghunm amesema:

”Nikamsimulia haya ´Uthmaan, Mu´aawiyah, Yaziyd na ´Abdul-Malik.”

Ameipokea Ibn Sammuuyah katika ”al-Fawaa-id”[1].

[1] Mtunzi wa kitabu ameipokea kupitia cheni yake ya wapokezi. ad-Daarimiy ameipokea kwa kifupi. Cheni zote za wapokezi ni Swahiyh. Wapokezi wake ni waaminifu ikiwa Sa´d bin ´Abdil-´Aziyz at-Tannuukhiy ameihadithia kabla ya kuanza kuchanganya kwake mambo. Hili la pili ndio lenye nguvu zaidi kwangu, kwa sababu Abu Mushir ndiye kapokea kutoka kwake, na yeye ndiye ambaye ameeleza kuhusu kuchanganyikiwa kwake. Dhana yangu kubwa ni kwamba hapokei kutoka kwake kutokana na kasoro yake hii, khaswa kwa kuzingatia kwamba anamtukuza sana. Abu Haatim ameeleza kwamba ”Abu Mashir alikuwa akimtanguliza mbele Sa´d bin ´Abdil-´Aziyz kabla ya al-Awzaa´iy”. Dhahiri ni kwamba hakuwa akifanya hivo isipokuwa kabla ya huyu kuanza kuyachanganya mambo. Kwa ajili hiyo kusimulia kutoka kwake hakukuwi isipokuwa katika hali kama hii – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 103
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy