Wanazuoni wengi wameona kuwa ni lazima kulipa siku ambayo kujamiiana kulitokea, kwa sababu ameiharibu siku yake ya Ramadhaan. Kwa hivyo analazimika kuilipa kama vile mtu anayeiharibu kwa kula. Kafara ni adhabu ya dhambi aliyofanya na kulipa ni mbadala wa siku aliyoiharibu[1]. Ibn Hazm na kundi jingine wameona kuwa haimpasi kulipa siku hiyo. Muwaffaq Ibn Qudaamah ametaja kuwa hii ni moja ya maoni ya ash-Shaafi´iy[2], kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumuamrisha bwama yule kulipa siku hiyo. Pia kwa kuwa alifanya kwa makusudi, basi hatolipa, kama njia ya kumfanya aadhibike zaidi na makosa yake. Haya ni maoni ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah ambaye amesema kuwa kila mwenye kuacha swalah au swawm kwa makusudi bila udhuru wowote, basi haifai kwake kulipa na wala haisihi kwake[3]. Mapokezi yanayosema:
“Funga siku moja badala yake.”
ni dhaifu, kama ilivyotangulia. Hata hivyo hapanaa shaka yoyote kuwa kulipa siku nyingine ndio salama zaidi na kutakasa dhimma ya mtu.
Inajuzu kwa mtu kuelezea hali yake ya ufukara ikiwa ni mkweli na asifanye hivyo kwa lengo la kulalamikia makadirio ya Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikubali maneno ya yule mtu kuhusu hali yake ya umasikini na hakumkemea.
Inajuzu kwa mtu kuapa juu ya jambo ambalo ana yakini nalo kwa dhana kubwa, kwani yule mtu alimwapia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba hakuna nyumba yoyote Madiynah iliyokuwa maskini zaidi kuliko yake, jambo ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkubalia, ijapokuwa hili si jambo linaloweza kujulikana kwa uhakika mara zote – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.
[1] at-Tamhiyd (07/157) na “al-Istidhkaar” (10/98).
[2] al-Muhallaa (06/264) na “al-Mughniy” (04/372).
[3] al-Ikhtiyaaraat”, uk. 109 na “Minhaaj-us-Sunnah (05/223-224).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/68)
- Imechapishwa: 17/03/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/68)
Imechapishwa: 17/03/2025
https://firqatunnajia.com/50-kafara-na-kulipa-siku-nyingine-au-kafara-pekee/