50. Du´aa ya kumshukuru Allaah baada ya kula na kunywa

133 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah anaridhia kwa mja kuwa anapokula mlo basi akamuhimidi kwacho au akanywa kinywaji basi akamuhimidi kwacho.”[1]

Ameipokea Muslim.

134 – Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:“Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pindi anapomaliza chakula chake husema:

الْحَمْـدُ للهِ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُبـارَكاً فيه، [غَيْرَ مَكْفِيٍّ] وَلا مُوَدَّعٍ وَلا مُسْتَغْـنىً عَنْـهُ رَبُّـنا

“Himdi zote njema anastahiki Allaah, himdi nyingi, nzuri, zenye baraka ndani yake [zisizorudishwa] wala kuagwa, wala kutoshwa nazo, Mola wetu.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

الحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي كَفَانَا وَأَرْوَانَا ، غَيْرَ مَكْفِي وَلَا مَكْفُورٍ ، وَقَالَ مَرَّةً : الحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّنَا ، غَيْرَ مَكْفِيٌّ وَلَا مُوَدَّعِ وَلَا مُسْتَغْنِّى ، رَبَّنَا

“Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ametutosheleza na kutupa tunachohitaji, zisizorudishwa wala kukanushwa.”

Mara nyingine akisema:

“Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wetu, zisizorudishwa wala kuagwa, wala kutoshwa nazo, Mola wetu.”[2]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna mapendekezo ya kumhimidi Allaah (´Azza wa Jall) wakati wa kula na kunywa na baada ya kula na kunywa. Jengine ni kwamba kufanya hivo ni miongoni mwa sababu za kumridhisha Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Muslim (2734).

[2] al-Bukhaariy (5458).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 11/11/2025