Ahl-us-Sunnah vilevile wako kati kwa kati inapohusiana na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baina ya Raafidhwah na Khawaarij. Raafidhwah wamevuka mipaka na Khawaarij wamezembea. Khawaarij wamewapiga vita Maswahabah na wakakufurisha wengi katika wao. Ama Raafidhwah wao wamevuka mipaka kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wao wanawatakia radhi Maswahabah wote (Radhiya Allaahu ´anhum), wanaamini kuwa wote ni waadilifu na kwamba wao ndio viumbe bora wa Allaah baada ya Mitume (´alayhimus-Swalatu was-Salam). Jengine ni kwamba wanajitenga mbali na mwenendo wa Raafidhwah ambao wamepetuka mipaka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) na watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na (Radhiya Allaahu ´anhum). Ahl-us-Sunnah hawavuki mipaka na hawazembei. Wao wako upande wa Maswahabah kwa kuwatakia radhi, wanaamini kuwa wao ndio viumbe bora baada ya Mitume na Manabii (´alayhimus-Swalatu was-Salam) na wanaamini kuwa wao ndio viumbe bora kabisa wa ummah huu. Pamoja na yote haya hawavuki mipaka kwao kama walivyofanya Raafidhwah kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) na watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale ambapo wanawaomba pamoja na Allaah na wanadai kuwa wamekingwa na kukosea. Yote haya si sahihi. Raafidhwah wamevuka mipaka na kupotea.
Khawaarij wao wamezembea inapokuja katika haki ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na hawakuthibitisha uadilifu wao.
Ahl-us-Sunnah wao wamethibitisha uadilifu wa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na fadhila zao na kwamba wao ndio viumbe bora baada ya Mitume (´alayhimus-Swalatu was-Salaam). Lakini hata hivyo wameenda kinyume na Raafidhwah katika kuchupa kwao mipaka. Hawakuvuka mipaka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) wala kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).´Aliy ni kama Maswahabah wengine wote (Radhiya Allaahu ´anhum). Yeye ni khaliyfah wa nne. Anazo fadhilah zake. Yeye ni mmoja katika wale Maswahabah kumi walioahidiwa Pepo. Hata hivyo haifai kwa mtu kuchupa mipaka kwake. Haitakiwi kumuomba pamoja na Allaah. Haitakiwi kusema kuwa amekingwa na kukosea, kwamba ndiye Mtume au kwamba Jibriyl (´alayhis-Salaam) alifanya khiyana katika Ujumbe. Yote haya ni batili. Lakini wanaona kuwa ni miongoni mwa Maswahabah wabora na wema – Allaah awawie radhi wote. Pamoja na yote haya hawavuki mipaka kwao, hawavuki mipaka kwa Faatwimah (Radhiya Allaahu ´anhaa), al-Hasan na al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na wengineo. Bali wanaonelea kuwa yule mwenye kufuata haki miongoni mwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye ambaye ana sifa za waumini, anastahiki kuombewa du´aa na kutakiwa radhi. Lakini hata hivyo hawavuki mipaka kwao. Wanazitambua fadhilah zao, kwamba wao ndio waislamu bora kabisa na wana nafasi yenye kujulikana mbele ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
Badala yake wanawatakia radhi, wanawaombea msamaha na wanaonelea mwenye kufuata haki miongoni mwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mwema na wanatarajia mema kwake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 72-73
- Imechapishwa: 24/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)