Ndoa sio mchanganyiko. Ndoa ni mu´amala wa milele. Mwanaume anavua nguo zake nyumbani kwake. Anaishi na mwanamke anayehitajia mahitajio yake kutoka kwake. Yeye pia anahitajia mahitajio yake kutoka kwake. Wote wanaishi maisha marefu. Haiwezekani yakafanywa kuwa ni yenye kutimizwa au kuwa imara, sahihi, yenye kuendelea na siku zote kuwa mapya kwa mapenzi kunjufu na furaha isipokuwa kwa dini na tabia njema. Mahusiano yote hupungua kidogo kidogo ikiwa hayakujengwa juu ya dini na tabia njema. Mahusiano kama hayo yanakuwa imara na safi na kila wakati wema na furaha ya wanandoa hao unakuwa mpya. Kwa ajili hiyo mpenzi wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke huolewa kutokana na [sababu] nne; kwa mali yake, nasabu yake, uzuri wake na kwa dini yake. Kwa hivyo oa mwanamke mwenye dini, mikono yako ifunikwe na udongo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amehamasisha kuoa mwanamke mwenye dini na kusema:
“Kila mmoja kati yenu ahakikishe ni mwenye moyo wenye kushukuru, ulimi wenye kukumbuka na mke muumini atayewasaidizeni kwa ajili ya Aakhirah.”[2]
Ukiwa na mambo haya matatu una kheri yote; moyo wenye kushukuru, ulimi wenye kukumbuka na mwanamke muumini mwema na mwenye dini atayekusaidia kwa ajili ya Aakhirah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dunia ni starehe na hakuna starehe ya dunia ilio bora kama mwanamke mwema.”[3]
Mshairi amesema
Msichana si yule mwenye uzuri wala mali
sivyo, wala si kwa fakhari ya mababu zake
Msichana ni yule mwenye utakaso, usafi wake na wema wake
kwa mume na watoto wake
[1] al-Bukhaariy (5090) na Muslim (1466)
[2] at-Tirmidhiy (3094), Ahmad (5/278) na Ibn Maajah (1856). Nzuri kwa mujibu wa at-Tirmidhiy na Ibn Hajar i ”al-Imtwaa´”, uk. 32. Tazama ”as-Swahiyhah” (2176) ya al-Albaaniy.
[3] Muslim (1467)
- Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 11-12
- Imechapishwa: 23/03/2017

Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 11-12
Imechapishwa: 23/03/2017
https://firqatunnajia.com/5-mwanamke-mwenye-kukusaidia-kwa-ajili-ya-aakhirah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)