205 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Abu Hudhwayfah ametukhabarisha, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Yuunus, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa ´Utayy, kutoka kwa Ubayy bin Ka´b, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ameifananisha dunia na mfano wa mwanadamu. Basi na aangalie mtu kinachotoka kwa mwanadamu, hata kama atakipamba na kukitia chumvi, mwishowe na aangalie kinavyoishilia.”[1]

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (382).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 53
  • Imechapishwa: 15/07/2025