49. Kutaja jina la Allaah kabla ya kuanza kula

132 – ´Umar bin Abiy Salamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia:

“Nilikuwa kijana katika uangalizi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mkono wangu ulikuwa ukizunguka ndani ya sahani. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanambia:

“Ee kijana! Taja jina la Allaah, kula kwa mkono wako wa kulia na kula kile kilichoko mbele yako.”

Kuanzia kipindi hicho hiyo ndio ikawa namna yangu ya kula.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

MAELEZO

Hadiyth hii inafahamisha uwekwaji Shari´ah wa adabu hizi tatu ambazo ni zifuatazo:

1 – Kutaja jina la Allaah kabla ya kula. Useme:

باسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

au:

بسم الله الرحمن الرحيم

“Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”

Kwa sababu Tasmiyah ni ishara ya:

بسم الله الرحمن الرحيم

“Kwa jina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”

2 – Kula kwa mkono wa kuume, jambo ambalo ni lazima. Hilo ni kutokana na Hadiyth inayosema:

“Hutoweza kamwe!”[2]

Hakuna kilichomzuia isipokuwa kiburi.

3 – Mtu akile kile kilicho mbele yake. Kwa maana nyingine asile kile kilichoko katikati ya sahani. Hapa ni pale ambapo chakula ni cha aina moja. Hapana vibaya ikiwa ni aina mbalimbali ya vyakula.

[1] al-Bukhaariy (5376) na Muslim (2022).

[2] Muslim (2021).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 128
  • Imechapishwa: 11/11/2025