Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
إِيَّاكَ نَعْبُدُ
”Wewe pekee ndiye tunakuabudu… ”[1]
Yaani hatumuabudu mwengine yeyote badala Yako. Hii ni ahadi iliopo baina ya mja na Mola Wake ya kwamba hatomuabudu mwengine asiyekuwa Yeye.
وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
“… na Wewe pekee ndiye tunakutaka msaada.”
Yaani ni ahadi iliopo baina ya mja na Mola Wake kwamba hatoomba msaada kwa mwengine asiyekuwa Yeye.
MAELEZO
Allaah (‘Azza wa Jall) amesema:
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
“Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.”[2]
Kutangulizwa kwa muktadha wa maneno sentesi:
إِيَّاكَُ
”Wewe pekee… ”
katika ´ibaadah na kuomba ulinzi kunaashiria upekee na maalum – upekee wa ´ibaadah kwa Allaah na maalum kwa ajili Yake. Kwa maana nyingine ni kwamba haabudiwi isipokuwa Allaah na hakuombwi msaada isipokuwa kwa Allaah. Mja haombi msaada kwa Malaika, majini wala viumbe visivoonekana. Ama kumuomba msaada binadamu aliye mbele yake, anayeweza kusaidia na kumsaidia kwa kumpatia manufaa au kuondoa madhara ni jambo linalofaa na halina ubaya wowote.
[1] 01:05
[2] 51:56
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 55-56
- Imechapishwa: 04/06/2026
Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
إِيَّاكَ نَعْبُدُ
”Wewe pekee ndiye tunakuabudu… ”[1]
Yaani hatumuabudu mwengine yeyote badala Yako. Hii ni ahadi iliopo baina ya mja na Mola Wake ya kwamba hatomuabudu mwengine asiyekuwa Yeye.
وإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ
“… na Wewe pekee ndiye tunakutaka msaada.”
Yaani ni ahadi iliopo baina ya mja na Mola Wake kwamba hatoomba msaada kwa mwengine asiyekuwa Yeye.
MAELEZO
Allaah (‘Azza wa Jall) amesema:
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
“Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.”[2]
Kutangulizwa kwa muktadha wa maneno sentesi:
إِيَّاكَُ
”Wewe pekee… ”
katika ´ibaadah na kuomba ulinzi kunaashiria upekee na maalum – upekee wa ´ibaadah kwa Allaah na maalum kwa ajili Yake. Kwa maana nyingine ni kwamba haabudiwi isipokuwa Allaah na hakuombwi msaada isipokuwa kwa Allaah. Mja haombi msaada kwa Malaika, majini wala viumbe visivoonekana. Ama kumuomba msaada binadamu aliye mbele yake, anayeweza kusaidia na kumsaidia kwa kumpatia manufaa au kuondoa madhara ni jambo linalofaa na halina ubaya wowote.
[1] 01:05
[2] 51:56
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 55-56
Imechapishwa: 04/06/2026
https://firqatunnajia.com/49-ibaadah-anafanyiwa-allaah-pekee/