46 – Qays amesimulia:

”Wakati ´Umar alipofika Shaam juu ya ngamia wake, watu walimpokea na wakasema: ”Ee kiongozi wa waumini! Endapo ungepanda farasi wa kazi, ukapokelewa na viongozi na watu wenye ngazi za juu.” Akasema: ”Nisikuonyesheni hapa? Amri inatokezea hapa” na akaashiria kwa mkono wake mbinguni.”[1]

Cheni ya wapokezi wake iko wazi kabisa.

[1] Ameipokea ad-Daarimiy, uk. 105, na katika “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 26. Na pia mtunzi kupitia kwake ambapo ameipokea. Cheni ya wapokezi ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy