48. Sura ya nne: Aina za unafiki na maelezo kuhusu unafiki wa kimatendo

Aina ya pili: Unafiki wa kimatendo. Ni kule kufanya kitu katika matendo ya wanafiki pamoja na kubaki imani ndani ya moyo. Unafiki aina hii haumtoi mtu nje ya Uislamu. Lakini hata hivyo ni njia inayopelekea katika hilo. Mwenye unafiki huyu anakuwa na imani na unafiki. Ukiwa mwingi basi kwa sababu yake anakuwa mnafiki safi. Dalili ya hayo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mambo manne mwenye kuyakusanya anakuwa ni mnafiki wa safi na ambaye ana sehemu katika hizo basi ana sehemu katika unafiki mpaka aziache; akiaminiw anafanya khiyana, anapozungumza husema uongo, anapoahidi hatimizi na anapogombana anafanya uovu.”[1]

Mwenye kukusanya sifa zote hizi nne basi amekusanya shari na amehitimisha sifa za wanafiki. Yule ambaye ana moja katika hizo basi ana sifa za unafiki. Mja anaweza kukusanya sifa za kheri na sifa za shari, sifa za imani na sifa za kufuru na unafiki. Mtu kama huyu anastahiki thawabu na adhabu kwa kiasi cha yale yanayopelekea katika jambo hilo.

Miongoni mwa sifa za kinafiki ni kufanya uvivu kutokamana na kuswali swalah ya mkusanyiko. Hii ni moja katika sifa za wanafiki. Kwa hivyo unafiki ni shari na ni khatari sana. Maswahabah walikuwa wakiogopa kutumbukia ndani yake. Ibn Abiy Mulaykah amesema:

“Nimekutana na Maswahabah thelathini wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wote walikuwa wanaogopa unafiki juu ya nafsi zao.”[2]

[1] al-Bukhaariy (34) na Muslim (207).

[2] Ameitaja al-Bukhaariy hali ya kuiwekea taaliki kwa njia ya kukata (01/146).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 92-93
  • Imechapishwa: 17/03/2020