Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

78 – Imani ni kule kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, siku ya Mwisho na makadirio, ya kheri na shari yake, tamu yake na chungu yake – yote yanatoka kwa Allaah (Ta´ala).

MAELEZO

Tambua kuwa haya hayapingani na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema:

”Kheri zote ziko mikononi Mwako na shari haitokani Nawe.”[1]

Hadiyth maana yake ni kwamba Allaah haumbi kitu kilicho na shari tupu, kila Anachokiumba kina hekima. Kwa njia hiyo ni kheri, lakini ndani ya kitu hicho kunaweza kuwa na shari kwa mtazamo kwa baadhi ya watu. Kwa hiyo shari hiyo ni ya sehemu na iliyoongezwa. Mola (Subhaanahu wa Ta´ala) ni Mwenye kutakasika na shari zote na ambazo hazikufungamana, kama alivobainisha Ibn Abiyl-´Izz al-Hanafiy. Yule anayetaka kuingia kwa ndani zaidi basi arejee katika ”Shifaa’-ul-´Aliyl” ya Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah). Humo utaona uwongo niliyonasibishiwa juu ya kwamba nimesema kuwa shari inayo muumba mwingine asiyekuwa Allaah (Ta´ala)[2].

[1] Muslim (771).

[2] Gazeti “al-Hadhwaarah”, uk. 50-52, 5/18.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 71-72
  • Imechapishwa: 06/10/2024