204 – Kathiyr bin ´Ubayd al-Hadhdhwaa’ ametukhabarisha: Marwaan bin Mu´aawiyah ametukhabarisha, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Shumaylah al-Answaariy, kutoka kwa Salamah bin ´Ubaydillaah bin Muhayswin al-Answaariy, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuamka salama nyumbani kwake, afya katika mwili wake na anacho chakula cha siku yake, basi ni kama vile ameimiliki dunia nzima.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (2346) na Ibn Maajah (4141). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2346).

  • Muhusika: Imaam Abu Bakr Ahmad bin Abiy ´Aaswim ash-Shaybaaniy (a.f.k. 287)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-uz-Zuhd, uk. 53
  • Imechapishwa: 15/07/2025