48. Du´aa ya msafiri anapoanza safari yake kabla ya afajiri

131 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapokuwa safarini na akaamka kabla ya alfajiri basi husema:

سَمِعَ سَامِعُ بِحَمْدِ اللَّهِ، وَحُسْنِ بَلَائِهِ عَلَيْنَا ، رَبَّنَا صَاحِبْنَا ، وَأَفْضِلْ عَلَيْنَا ، عَائِدًا بِاللَّهِ مِنَ النَّارِ

“Amesikia msikilizaji himdi za Allaah, uzuri wa mtihani Wake kwetu, Mola wetu ndiye Muhifadhi wetu, akatufadhilisha hali ya kuwa ni wenye kujilinda Kwake kutokana na Moto.”[1]

Ameipokea Muslim.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna du´aa ya msafiri anapoamka kabla ya alfajiri, ikiwa na maana ya mwisho wa usiku.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mola wetu ndiye Muhifadhi wetu… “

Bi maana anayetuhifadhi na anayetusimamia.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… akatufadhilisha… “

Kwa neema Zake kunjufu na akatuondoshea kila kinachochukiza.

Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… hali ya kuwa ni wenye kujilinda Kwake kutokana na Moto.”

Bi maana hali ya kuwa ni wenye kujilinda kwa Allaah kutokana na Moto.

[1] Muslim (2718).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 127
  • Imechapishwa: 10/11/2025