51. Du´aa ya mgonjwa ambaye amekata tamaa ya kuishi tena

  Download

150-

أللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي وَارْحَمْـني وَأَلْحِقْـني بِالرَّفـيقِ الأّعْلـى

”Ee Allaah! Nisamehe, unirehemu na unikutanishe na waja walio katika daraja za juu.”[1]

151-

”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anataka kukata roho alikuwa akiingiza mikono yake ndani ya maji kisha akipangusa kwayo uso wake na akisema:

لاَ إِلَهَ إِلاَّ الله، إِنَّ لِلْمَـوْتِ لَسَكَـراتٍ

”Hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah, hakika kifo kina uchungu.”[2]

152-

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَاللّهُ أَكْبَـر، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَريكَ لهُ، لا إلهَ إلاّ اللّهُ لهُ المُلكُ ولهُ الحَمْد، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَلا حَـوْلَ وَلا قُـوَّةَ إِلاّ بِالله

Hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa, hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah Mmoja pekee, hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah, ufalme ni Wake na himdi ni Zake, hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”[3]

[1] al-Bukhaariy (07/10) na Muslim (04/1893).

[2] al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (08/144) na katika Hadiyth ya Siwaak.

[3] at-Tirmidhiy na Ibn Maajah. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy. Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/152) na “Swahiyh Ibn Maajah” (02/317).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 01/05/2020