al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ
“Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika?”[1]
“Jaabir ameeleza kwamba Abu Ja´far amesema kuhusu Aayah hiyo: “Atashuka katika matao saba ya nuru pasi na yeyote kujua ni lipi katika hayo na ni pindi ataposhuka Kuufah.”
Abu Hamzah ameeleza kwamba Abu Ja´far amesema:
“Abu Hamzah! Ni kana kwamba namuona al-Qaa´im[2] wangu anapaa Najaf. Atapopaa Najaf atachukua bendera ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pindi atapoichukua Malaika wa Badr watamteremkia.”[3]
Namna hii ndivyo maadui wa Allaah wanavyoikengeusha Qur-aan. Ndani ya Aayah kuna khabari na maelezo ya kweli juu ya ujio wa Allaah kuwahukumu viumbe na kushuka kwa Malaika siku ya Qiyaamah. Waongo wanaipotosha na kusema kwamba inahusiana na ujio wa pumba zao walizozusha kwa ajili ya kupiga vita Uislamu na waislamu.
Tazama jinsi wanavyounyanyua mji wao wa kishaytwaan Najaf! Huko shaytwaan na majeshi yake yameshuka na kunyanyua bendera yake tangu hapo yalipodhihiri madhehebu ya Raafidhwah na wapukaji.
[1] 02:210
[2] al-Mahdiy.
[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/102).
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 80
- Imechapishwa: 03/04/2017
al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ فِي ظُلَلٍ مِّنَ الْغَمَامِ وَالْمَلَائِكَةُ
“Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie katika vivuli vya mawingu pamoja na Malaika?”[1]
“Jaabir ameeleza kwamba Abu Ja´far amesema kuhusu Aayah hiyo: “Atashuka katika matao saba ya nuru pasi na yeyote kujua ni lipi katika hayo na ni pindi ataposhuka Kuufah.”
Abu Hamzah ameeleza kwamba Abu Ja´far amesema:
“Abu Hamzah! Ni kana kwamba namuona al-Qaa´im[2] wangu anapaa Najaf. Atapopaa Najaf atachukua bendera ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pindi atapoichukua Malaika wa Badr watamteremkia.”[3]
Namna hii ndivyo maadui wa Allaah wanavyoikengeusha Qur-aan. Ndani ya Aayah kuna khabari na maelezo ya kweli juu ya ujio wa Allaah kuwahukumu viumbe na kushuka kwa Malaika siku ya Qiyaamah. Waongo wanaipotosha na kusema kwamba inahusiana na ujio wa pumba zao walizozusha kwa ajili ya kupiga vita Uislamu na waislamu.
Tazama jinsi wanavyounyanyua mji wao wa kishaytwaan Najaf! Huko shaytwaan na majeshi yake yameshuka na kunyanyua bendera yake tangu hapo yalipodhihiri madhehebu ya Raafidhwah na wapukaji.
[1] 02:210
[2] al-Mahdiy.
[3] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (01/102).
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 80
Imechapishwa: 03/04/2017
https://firqatunnajia.com/48-al-ayyaashiy-upotoshaji-wa-kumi-na-saba-wa-al-baqarah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)