Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Amewaamrisha pia kumdhukuru Allaah. Mfano wake ni kama mtu aliyetafutwa na adui kwa kasi mpaka akafikia ngome madhubuti, basi akajikinga humo nao. Hali kadhalika mja hajilindi dhidi ya shaytwaan isipokuwa kwa kumtaja Allaah (Ta´ala).”

Lau haikuwapo katika Dhikr isipokuwa sifa hii moja, basi ingelitosha kabisa kwa mja kutoacha ulimi wake daima kumtaja Allaah (´Azza wa Jall) na awe daima na mazoea ya kumtaja Allaah. Kwa sababu hawezi kujiweka salama na adui yake isipokuwa kwa Dhikr na adui hawezi kumpata isipokuwa kwa njia ya kughafilika. Hivyo shaytwaan humvizia na anapoghafilika humrukia na kumuangamiza. Anapomdhukuru Allaah (´Azza wa Jall) adui wa Allaah hugeuka, kujificha na kudhalilika hadi awe kama ndege mdogo au kama inzi. Kwa ajili hii wasiwasi umepewa jina la kuwatia watu wasiwasi, kwa maana ananong’ona kutia wasiwasi vifuani, lakini anapomtaja Allaah (Ta´ala) hukoma na hukandamizwa. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Shaytwaan hukaa amekalia juu ya moyo wa mwanadamu. Anapoghafilika na kusahau, anamnong’ona, na anapomtaja Allaah (Ta´ala), basi hugeuka nyuma.”[1]

[1] Ibn Abiy Shaybah (13/369-370).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 83
  • Imechapishwa: 17/08/2025