Hadiyth hii ni dalili kwamba mwenye kujamiiana ndani ya mchana wa Ramadhaan, basi analazimika kutoa kafara kubwa zaidi, ambayo imepangwa kwa mpangilio ufuatao:
1 – Kuacha huru mtumwa. Na dhahiri ya Hadiyth ni kwamba haishurutishwi kuwa ni muumini, kwa sababu imeachwa wazi bila ya kuainishwa kwa imani, ambayo ni maoni ya Hanafiyyah. Wanazuoni wengi wameshurutisha mtumwa awe muumini, kwa njia ya kufasiri yaliyoachiwa kwa zile zilizofungamanishwa, kwa kuwa Allaah Ameshurutisha imani katika kafara ya kuua mtu, ijapokuwa sababu ni tofauti.
2 – Asiyepata mtumwa, basi afunge miezi miwili mfululizo bila ya kukatizwa na kula, isipokuwa kutokana na udhuru kama ugonjwa na mfano wake.
3 – Asiyeweza, basi atoe chakula kwa masikini sitini.
Haya ndio maoni ya wanazuoni wengi katika Salaf na waliokuja baadaye. Ama yaliyopokelewa kutoka kwa ash-Sha´biy, an-Nakha´iy na Sa´iyd bin Jubayr kwamba inampasa kufidia kwa kufunga tu bila ya kafara, hili linatokana na kwamba Hadiyth haikuwafikia, kama alivyosema al-Baghawiy[1]. Kafara hii imekhusishwa kwa kujamiiana ndani ya Ramadhaan. Kwa msemo mwingine akijamiiana katika siku ya kulipa Ramadhaan, swawm yake inabatilika na itampasa kuilipa lakini hana kafara, kwa sababu kafara ni maalum kwa ajili ya Ramadhaan kwa kuwa ina heshima maalum na kula ndani yake ni kuivunjia heshima hiyo, tofauti na kula katika siku ya kulipa, kwani siku hizo ni sawa kwake.
[1] Shar-us-Sunnah (06/284).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/65-66)
- Imechapishwa: 16/03/2025
Hadiyth hii ni dalili kwamba mwenye kujamiiana ndani ya mchana wa Ramadhaan, basi analazimika kutoa kafara kubwa zaidi, ambayo imepangwa kwa mpangilio ufuatao:
1 – Kuacha huru mtumwa. Na dhahiri ya Hadiyth ni kwamba haishurutishwi kuwa ni muumini, kwa sababu imeachwa wazi bila ya kuainishwa kwa imani, ambayo ni maoni ya Hanafiyyah. Wanazuoni wengi wameshurutisha mtumwa awe muumini, kwa njia ya kufasiri yaliyoachiwa kwa zile zilizofungamanishwa, kwa kuwa Allaah Ameshurutisha imani katika kafara ya kuua mtu, ijapokuwa sababu ni tofauti.
2 – Asiyepata mtumwa, basi afunge miezi miwili mfululizo bila ya kukatizwa na kula, isipokuwa kutokana na udhuru kama ugonjwa na mfano wake.
3 – Asiyeweza, basi atoe chakula kwa masikini sitini.
Haya ndio maoni ya wanazuoni wengi katika Salaf na waliokuja baadaye. Ama yaliyopokelewa kutoka kwa ash-Sha´biy, an-Nakha´iy na Sa´iyd bin Jubayr kwamba inampasa kufidia kwa kufunga tu bila ya kafara, hili linatokana na kwamba Hadiyth haikuwafikia, kama alivyosema al-Baghawiy[1]. Kafara hii imekhusishwa kwa kujamiiana ndani ya Ramadhaan. Kwa msemo mwingine akijamiiana katika siku ya kulipa Ramadhaan, swawm yake inabatilika na itampasa kuilipa lakini hana kafara, kwa sababu kafara ni maalum kwa ajili ya Ramadhaan kwa kuwa ina heshima maalum na kula ndani yake ni kuivunjia heshima hiyo, tofauti na kula katika siku ya kulipa, kwani siku hizo ni sawa kwake.
[1] Shar-us-Sunnah (06/284).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/65-66)
Imechapishwa: 16/03/2025
https://firqatunnajia.com/46-yanayompasa-mfungaji-aliyejamiiana-mchana-wa-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket