Tambueni kwamba ni wajibu juu yenu kuzijua hukumu za kulipa kwa yule aliyekula katika mchana wa Ramadhaan kutokana na udhuru miongoni mwa udhuru unaokubalika katika Shari´ah. Amesema (Ta´ala):
وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ
”Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi [atimize] idadi katika siku nyinginezo. Allaah anakutakieni mepesi na wala hakutakieni magumu. [Fungeni siku mlizowekewa] ili mkamilishe idadi.”[1]
Mwishoni mwa Aayah hii Tukufu Allaah ametoa ruhusa ya kufungua ndani ya Ramadhaan kwa mgonjwa na msafiri na amewalazimisha kulipa iwapo watatumia ruhusa hiyo na wakafungua; kwa kufunga idadi ya siku walizofungua katika mwezi mwingine. Wakifunga Ramadhaan bila kutumia ruhusa hiyo, basi swawm yao ni sahihi na inatosheleza kwa mujibu wa jopo kubwa la wanazuoni, maoni ambayo ndio ya haki. Amebainisha (Subhaanah) hekima ya ruhusa hii; nayo ni kwamba Alitaka kuwaletea wepesi waja Wake wala hakutaka kwao uzito na mashaka kwa kuwakalifisha swawm katika hali ya safari na maradhi. Na kwamba hekima ya kuwajibisha kulipa ni kutimiza idadi ya siku alizowajibisha Allaah kufungwa. Katika ruhusa hii kumejumuishwa kuleta wepesi na kutimiza idadi inayotakiwa kufungwa.
Kuna kundi la tatu ambalo limepewa ruhusa ya kula, nao ni mzee aliyechakaa sana na mgonjwa mwenye maradhi sugu ikiwa hawawezi kustahimili funga. Amesema (Ta´ala):
وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ
“Na ni juu ya wale wanaoiweza [kufunga swawm] lakini kwa tabu watoe fidia kulisha masikini.”[2]
Maana ya wanaoimudu (يطيقونه) wanaiweza kwa taabu na inawapa mashaka. Kwa hiyo ni juu yao badala ya swawm ni kumlisha chakula masikini kwa kila siku iliyowapita. Hili ni kwa mujibu wa aliyoyasema jopo la wanazuoni katika kufasiri Aayah hii na kwamba haikufutwa. Hukumu hiyohiyo inamuhusu mjamzito na anayenyonyesha iwapo watakhofia juu ya nafsi zao wenyewe au juu ya watoto wao kutokana na kufunga. Hivo ndivo ilivyopokelewa kutoka kwa Ibn ´Abbaas kwamba alimwambia mama wa mtoto wake aliyekuwa mjamzito au anayenyonyesha:
”Wewe ni kama wale wasioweza kustahimili swawm.”
Vilevile imepokelewa kwamba mmoja wa wasichana wa Ibn ´Umar alimtumia ujumbe akimuuliza kuhusu swawm ya Ramadhaan hali yeye ni mjamzito ambapo akasema:
”Afungue na amlishe chakula masikini kwa kila siku iliyompita.”
Hawa wote wanaruhusiwa kula katika mchana wa Ramadhaan kwa kuzingatia udhuru wao wa Kishari´ah.
[1] 02:185
[2] 02:184
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 44
- Imechapishwa: 17/03/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 44
Imechapishwa: 17/03/2026
https://firqatunnajia.com/46-watu-waliopewa-ruhusa-ya-kula-ramadhaan/