Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Siku moja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipanda juu ya mimbari na kuita kwa sauti ya juu:  ”Enyi kundi la mlioamini kwa ulimi wao na bado imani haijaingia katika nyoyo zao! Msiwaudhi waislamu na wala msifuatilie aibu zao! Kwani hakika anayefatilia aibu ya ndugu yake, basi Allaah humfuatilia aibu yake. Na Allaah anapomfuatilia mtu aibu yake, basi humfedhehesha hata akiwa ndani ya nyumba yake.”[1]

Ameipokea at-Tirmidhiy.

Unavuna kile ulichopanda. Kuwa kama unavyotaka – Allaah (Ta´ala) anakuwa kwako vile unavyokuwa Kwake na kwa waja Wake.

Wakati wanafiki walipoonyesha unafiki na wakaficha ukafiri, Allaah (Ta´ala) akawaonyesha nuru juu ya Njia na akawavizia kwamba wataweza kupita, lakini akaficha kwao kuwa atawazima nuru yao na atawazuia wasivuke. Watavuna kile walichopanda.

Vivyo hivyo yule anayewaonyesha watu hali ya nje tofauti na kile ambacho Allaah (Ta´ala) anamjua kwacho, basi Allaah humfunulia njia za kufaulu, ustawi na ushindi duniani na Aakhirah huku akificha kinyume chake. Imekuja katika Hadiyth:

”Anayetenda kwa kujionyesha, basi Allaah atamfanya kuwa wa kuonekana na anayesikilizisha watu, basi Allaah atamsikilizisha.”[2]

Makusudio ni kwamba mtu mkarimu na mwenye kutoa, Allaah humlipa na kumpa zaidi ya yule asiyetenda kwa namna hiyo – anapata kutokana na vile alicholima.

[1] at-Tirmidhiy (2032). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (2032).

[2] al-Bukhaariy (6499) na Muslim (93).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 81-82
  • Imechapishwa: 13/08/2025