Mapote matatu ndio yenye uadui kwa Maswahabah:
1 – Raafidhwah.
2 – Khawaarij.
3 – Naaswibah.
Lakini hata hivyo wabaya zaidi ni Raafidhwah.
Kilichowapelekea Khawaarij kufanya hivi ni kuwa na ususuwavu na kupetuka mipaka katika dini. Hawa malengo yao haikuwa kuutukana Uislamu. Walifanya hivi kwa sababu ya kupetuka mipaka na ususuwavu katika dini. Lengo lao haikuwa kuitukana dini. Bali haya – kwa madai yao – ni kwa sababu ya kuipenda kwao dini na kuipupia.
Kuhusu Nawaaswib kilichowapelekea kuwatukana baadhi ya Maswahabah ni kwa sababu ya jambo la kisiasa. Wanachotaka kwa kufanya hivo ni kutukana uongozi wa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Sababu ilikuwa jambo la kisiasa tu na kwamba hastahiki uongozi. Malengo yao pia haikuwa kuitukana dini.
Lakini kuhusu Raafidhwah – Allaah awatweze – malengo yao ilikuwa kuitukana dini. Endapo watawasema vibaya na kuwatukana Maswahabah, basi kutakuwa hakukubaki baina yetu sisi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ukati na kati wowote ilihali dini imetufikia kupitia njia ya Maswahabah ambao – kwa mtazamo wa Raafidhwah – maneno yao hayatumiwi kama hoja. Kwa hivyo huku ni kuitukana dini. Haya ndio malengo yao.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 113
- Imechapishwa: 10/01/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)